Kuna habari kuwa msanii Hussein Ramadhani Mkiety liyekuwa
maarufu kwa jina la Sharo Millionea, msanii wa muziki na maarufu katika
kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia
baada ya kupata ajali ya gari Tanga.
Kamanda
wa Polisimkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa
Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza
ambapo pia ndio nyumbani kwao
R.I.P SHARO MILLIONEA
Alichosema kamanda hichi kama umeshinda kuisikiliza
Kuhusu
kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi
Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera
Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo
Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea
Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia
na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda
amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu
aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari
imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.