kabesejr blog
kabesejr
albino
Sunday, April 7
BEN POL, LINAH NA BINTI MACHOZI KUNANI?
UNAJUA kinachoendelea katika mitandao ya kijamii? Leo nazungumza na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, Benard Paul ‘Ben Pol’ na Estelina Sanga ‘Linah’.
Kwako wewe the big boss wa Machozi Band, Jide au Anaconda kama unavyojiita siku hizi. Katika siku za hivi karibuni umekuwa ukilalama sana kuhusu kubaniwa kupigwa kwa ngoma yako mpya ya Joto Hasira na kituo kimoja cha redio.
Hilo sitalijadili kwa kuwa wewe siyo wa kwanza kulalamika. Kama vipi jiunge na harakati za vinega kitaeleweka tu kwa kuwa umeamua kuingia kwenye vita, nina uhakika umejiandaa.
Baada ya sakata hilo, uliamua kugeuza kibao, mashambulizi ukayaelekeza kwa Ben Pol na Linah.
Kupitia akaunti yako ya Twitter uliwashambulia wadogo zako hao ukidai kuwa walikusaliti. Ulidai kuwa walikatazwa na bosi wao kufanya shoo hapo mgahawani kwako, Nyumbani Lounge licha ya kulipwa kianzio.
Uliandika: “Linah na Ben Pol mnabisha hamkukatazwa? Nisalitini ila hamtapata faida, mtatoka kapa pia.”
Ni kweli uliwatuhumu vibaya mno bila ushahidi. Mzigo wa tuhuma ukapokelewa kwa hasira na Ben Pol. Akakujibu kwa maneno makali bila kujali umri na ukongwe wako kwenye gemu.
Akakujibu: “Hiyo show kulikuwa na wengine pia waku-perform, je, waliperform? Kama nililipwa nikashindwa ku-show up, mbona sidaiwi?? Tafakari.”
Aliendelea kukuza mambo naye bila ushahidi: “Ben Pol hana muda wa maneno na majungu. Ombi langu ni moja kwako. Put me out of your business. Period!”
“Don’t talk about things you don’t know about. Don’t.”
Ben Pol akaendelea kuchana: “Ukiwaza kutumia akili kamwe huwezi kukosea, ila utakapotumia hisia lazima ujikanyage somewhere. Nimekua vya kutosha. Trust me.”
Kama hukuweza kuyapitia maoni ya mashabiki wako, nitakusaidia. Wengi walionesha kusikitishwa kwa kitendo chako huku wakikutaka kufuata taratibu ili mambo yaende sawa.
Ulichokifanya kimesababisha mashabiki wako waanze kuhisi kuwa kuna kitu kikubwa kinakuja katika muziki wa Bongo Fleva.
Mabishano yanayoendelea kati yako na kituo cha redio kinachokubania na sasa sakata lako na wasanii ambao ni wadogo zako, vinaleta picha kuwa huko tunakoelekea kuna anguko kubwa. Aidha, litakuhusu wewe kama mwanamuziki au tasnia nzima ya muziki wa Bongo Fleva. Ni aibu tupu!
Ulichotakiwa kufanya ni kufuata utaratibu, kukaa mezani au kufuata sheria kuliko malumbano ambayo yanalenga kukuondolea heshima uliyojijengea kwa zaidi ya miaka kumi kwa siku moja.
Ben Pol na Linah ni wadogo zako, wanategemea uwalee kisanii kwa kuwa wewe ndiye mwanamuziki pekee wa kike Bongo mwenye mafanikio kuliko wote. Kuna kila sababu ya kujisafisha kwa kukaa mezani na kuondoa aibu hii. Nimemaliza dada Jide ngoja nizungumze na Ben Pol kidogo.
Pamoja na hasira uliyokuwa nayo, Ben Pol hukupaswa kutumia maneno makali kwa dada yako, ni utovu wa nidhamu hata kama alikukosea. Ndiyo kusema Linah amekuzidi kwa busara? Kimya hutafsirika zaidi kuliko maneno. Tuchunge tunapoelekea. La sivyo, Bongo Fleva itakufa kutokana na chuki inayoendelea kukua kwa kasi kati ya msanii na msanii. For the love of game!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment