kabesejr blog

kabesejr

albino

Wednesday, July 31

BOSI WA HOME SHOPPING CENTRE HALI TETE



HALI ni tete kuhusiana na tukio la bilionea Said Mohamed Saad kumwagiwa tindikali, athari ni kubwa. Jinsi alivyoharibika inatia simanzi lakini kumpata mhusika wa unyama huo ni kitendawili kinacholitega Jeshi la Polisi Tanzania.
 
Rais Kikwete akimjulia hali mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad.
Said ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Centre, yenye maduka mengi makubwa ya vitu vya nyumbani ndani ya Dar es Salaam na mikoa kadhaa ya Tanzania, anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini lakini mmoja wa watu waliomshuhudia, amefafanua jinsi hali ilivyo mbaya.
“Ameungua sana, tunatarajia kati ya kesho au keshokutwa (wikiendi iliyopita) atafanyiwa oparesheni ya jicho. Jamani tindikali ni mbaya sana, usimmwagie mwenzako. Ndugu yetu ameharibika sana,” kilisema chanzo chetu kwa ombi la kutotajwa jina gazetini, kikaongeza:
“Kila anayemjua vizuri, anapomwona anamwaga machozi. Picha za jinsi alivyoathirika baada ya kumwagiwa tindikali zimevuja mpaka kwa familia, ni kilio kwa ndugu. Wanawake wanalia zaidi.”

JK ATINGA HOSPITALI
Wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC).
Mkutano huo ni wa Pande Tatu za SADC (Troika of SADC) na akiwa huko, alipata fursa ya kwenda kumjulia hali katika hospitali aliyolazwa ambayo haijajulikana jina.
Chazo chetu kilisema: “Rais Kikwete alisikitika sana. Wakati anatoka wodini alisonya. Alionesha jinsi alivyosikitishwa na unyama aliotendewa Said.”
Bilionea Said Mohamed Saad akiwa hospitali.
WAPELELEZI WAMWAGWA KARIAKOO
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura aliwaambia waandishi wetu wiki iliyopita kwamba jeshi linaendelea kufanya kazi yake kuhakikisha linampata mhusika wa unyama huo.
“Mpaka sasa tuseme ukweli hatujampata mtuhumiwa au kitu kinachoonesha mtuhumiwa alivyo lakini kazi inafanyika. Tupo makini kwelikweli na tumeweka mkazo wa hali ya juu,” alisema Wambura.
Kwa upande mwingine, chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi kimehabarisha kuwa idadi kubwa ya wapelelezi wamemwagwa Kariakoo, Dar es Salaam.
“Kuna mambo yanazungumzwa kuhusiana na tukio la Said kumwagiwa tindikali, yanafanyiwa kazi. Kutokana na ukweli kwamba msingi wa biashara za Said ni Kariakoo, vilevile kwa sababu inatambulika kuwa eneo hilo lina wafanyabiashara wengi, imebidi kulimulika kwa undani kabisa.
“Inawezekana ni chuki za kibiashara. Yaani aliyemtendea, ama alimshambulia au alifanya kulipa kisasi kutokana na vita ya kimaslahi. Hili suala tunaliangalia kwa upana sana ndiyo maana wapelelezi wamemwagwa Kariakoo.
“Wanachunguza kila taarifa. Kila kinachozungumzwa kinafanyiwa kazi na wale ambao itaonekana upo ulazima wa kuwakamata, watakamatwa ili kuisaidia polisi kufanikisha kumpata mtu ambaye alihusika na kummwagia tindikali yule bwana wa Home Shopping Centre,” kilisema chanzo chetu.

DAR YOTE INAPELELEZWA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, pamoja na upelelezi kuwekewa mkazo Kariakoo lakini kazi ya kumsaka mhalifu aliyemfanyia unyama Said, inafanyika ndani ya jiji lote la Dar es Salaam pamoja na mikoa ambayo taarifa zitaelekeza.
“Kipindi chote ambacho upelelezi unafanyika, pengine zitaibuka taarifa zinazoelekeza mikoani ili kumpata mtuhumiwa, polisi watafika kote. Ukweli ni kwamba siyo tukio hili tu, jeshi la polisi limekuwa imara kufanyia kazi kila aina ya uhalifu.
“Pamoja na ugumu wa kumpata mtu hasa aliyemmwagia tindikali kutokana na mazingira yalivyokuwa, hilo halifanyi tukae kimya na tuache hili suala lipite. Maisha ya watu yanathaminiwa sana, unyama wa kuwadhuru wengine kwa vitu hatari kama tindikali, haukubaliki ndani ya polisi,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Maswali kuhusu aliyemmwagia tindikali hiyo, nani mhusika pamoja na sababu ya huyo aliyemmwagia tindikali, pengine ni mambo ambayo yanahitaji muda zaidi. Polisi wafanye kazi, mafanikio yake, yatatanzua utata wote.”

SHEMEJI MTU ATAJWA
Huku upelelezi ukiendelea, zipo taarifa kwamba mtu mmoja anayedaiwa kuwa shemeji wa Said, anatakiwa kuhojiwa kwani alishawahi kuripotiwa kuwa na uhusiano mbaya.
Ilibainishwa kwamba kumpata mhusika wa unyama huo, ni lazima kila aliyewahi kuripotiwa kuwa na tofauti za kijamii au kibiashara na Said, akamatwe na ahojiwe ili kuisaidia polisi.
“Yule shemeji yake ilishaelezwa waligombana sana. Mitandao ya kijamii ikaandika sana. Polisi hawatakiwi kudharau taarifa. Wamfuatilie huyo shemeji mtu, ahojiwe kwa makini,” alisema mfanyabiashara mmoja wa Kariakoo (jina tunalo), akaongeza:
“Siyo huyo shemeji yake peke yake, hata watu wengine wenye historia ya kugombana na Said, nao pia wamulikwe. Hili jambo ni nyeti, tena zito sana. Kumtenda binadamu ukatili wa kiwango hicho ni suala ambalo haliwezi kuvumilika.”

BODABODA TISHIO KWA NCHI
Said, alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu akiwa kwenye moja ya maduka yake katika Jengo la Msasani Mall, Dar ambalo nalo inadaiwa yeye ndiye analimiliki.
Taarifa za siku ya tukio zilibainisha kwamba Said alikuwa akizungumza na mfanyakazi wake mishale ya saa 1 jioni ndipo akatokea kijana mrefu, mwembamba ambaye alimmwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.
Ilibainishwa kwamba mfanyakazi huyo wa Said, Hassan Ahmad naye alijeruhiwa kidogo katika purukushani hiyo lakini alipopelekwa Hospitali ya Ami Wellness Centre, alitibiwa na kuruhusiwa huku bosi wake akipelekwa Afrika Kusini usiku huohuo.
Kwa vile mtu aliyemmwagia tindikali Said alifika eneo la tukio na pikipiki, Kamanda Wambura (RPC Kinondoni), alisema kuwa uhalifu kwa njia ya usafiri huo ni mkubwa sana, kwa hiyo kuna taarifa inaandaliwa.
“Uhalifu wa pikipiki hususan bodaboda ni tishio kwa nchi yetu kwa sasa, kuna taarifa inaandaliwa na itatolewa baadaye kuhusiana na mwongozo wa usafiri huo pamoja na namna ambavyo kama nchi, tutakabiliana na uhalifu kwa njia ya bodaboda.
“Kwa sasa mamlaka husika zinakaa. Zinajadili, siyo suala la kupuuza kabisa. Majambazi sasa wanatumia pikipiki, tunashuhudia kwamba hata watu wanaotaka kutekeleza njama za mauaji, nao wanatumia bodaboda. Ni hatari sana,” alisema Wambura.

BARUA NZITO TOKA KWA PAPII KOCHA KWA JK

Na Mwandishi Wetu
ULE waraka wa mwanamuziki aliyefungwa gerezani kifungo cha maisha sambamba na baba yake mzazi, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ umeibua mjadala tena huku Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiombwa na kukubali kuufikisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ (kushoto) akiwa na baba yake Nguza Viking ‘Babu Seya’.
MIAKA 10 GEREZANI
Hivi karibuni wasanii hao walitimiza miaka kumi tangu walipofungwa katika Gereza la Ukonga, Dar mwaka 2003 hivyo kusababisha waraka huo aliouandika Papii Kocha Februari mwaka 2010 kusababisha mjadala upya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Julai 21, mwaka huu waraka huo ulikuwa gumzo kubwa juu ya ombi la Papii Kocha kwa Rais Kikwete kuwa amhurumie atoke gerezani kwa kuwa bado ni kijana mdogo huku nyuma yake watu wakituhumiana bila ushahidi.
 
Waraka alioandika Papii Kocha kwa Mhe rais Kikwete.
OMBI KWA WAZIRI NYALANDU

MBUNGE WA KINONDONI NA KASHFA YA MADAWA YA KULEVYA,ATINGA POLISI

KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.

“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.

Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.

“Kila kinapofika kipindi kama hiki huwa kuna vuguvugu la uchaguzi, hivyo maneno kama haya husemwa ili kuharibiana sifa, nimewataka polisi wanichunguze na watakachokipata watoe taarifa kwa wananchi,” alisema.

Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.

Hata hivyo, Mbunge huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa hausiki kwa njia moja ama nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe jina lake kamili, namba yake ya ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa nchini ili ukweli ujulikane.

Thursday, July 25

AFUMANIWA NA KUKATWA MIGUU YOTE MIWILI BAADA YA KUNASWA AKILA URODA NA MKE WA MTU


Damu: Miguu ya Said Iddi ikivuja damu baada ya kukatwa.
Na Mwandishi Wetu, Kilosa
ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said  Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.
Mke wa mtu sumu: Said  Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini hapo.
MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.
“Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Chini ya ulinzi: Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.
Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.
MPANGO WA FUMANIZI

Monday, July 22

WEMA AJINAJISI MWEZI MTUKUFU



WAKATI zilipendwa wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifuturisha kila kukicha, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametupiwa madongo mazito akiambiwa amejinajisi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuatia picha zake  zisizopendeza kipindi cha mfungo kutumbukizwa mtandaoni, Ijumaa Wikienda linakupa habari kamili.
 
Moja ya picha alizotupia Wema Sepetu.
Julai 19, mwaka huu (Chungu cha Kumi) picha za Wema ambaye ni staa wa filamu za Bongo na Miss Tanzania mwaka 2006/07 ziliingizwwa mtandaoni akiwa katika mapozi mbalimbali yenye ‘kuuchefua’ mwezi kama mtu atakumbana nazo.
Picha moja ilimuonesha mrembo huyo akiwa ‘klozidi’ na meneja wake, Martin Kadinda. Wanaonekana wamekumbatiana.
Picha nyingine inamuonesha Wema akipiga mbizi kwenye swimming pool moja ambayo haikufafanuliwa ni wapi nchini Tanzania.
Mbali na picha hizo mbili, nyingine ilimuonesha mlimbwende huyo akiwa katika gauni jepesi kiasi cha kuweza kuonesha ‘nido’ zake.
Diamond (wa pili kulia) akifuturu na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Bongo.
WACHANGIAJI SASA
“Dah! Nimemshangaa sana Wema, amekubali vipi kuweka picha zake kwenye neti katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, maana hazistahili kabisa,” alisema mmoja wa wasomaji wetu ambaye  alibahatika kuziona picha hizo.
Msomaji huyo aliendelea kusema kwamba kwa uzoefu wake kipindi hiki cha mfungo ‘blogi’ nyingi (akimaanisha mitandao) zinaweka picha za watu wakifuturu, wengine wakifuturisha, alimshangaa Wema ni Muislamu safi lakini kumbe si mfuataji wa maadili ya imani.
“Wema amejinajisi tu kwa Mwezi wa Ramadhani, picha zilizoko kwenye mtandao siyo kabisa, ikiwezekana azitoe ataziweka tena baada ya mfungo kwisha,” alimalizia kusema mtu huyo.
Wachangiaji wengine hawakuwa mbali sana na wa kwanza, nao walionesha kukerwa kwao na jinsi picha hizo zilivyotupiwa mtandaoni katika kipindi hiki cha toba na kusema funga ya Wema ni bure.
 
Diamond katika vazi la kanzu.
AWALI YA YOTE
Kabla ya kumsaka Wema, Ijumaa Wikienda lilijiridhisha kwamba, mtandao uliotumika kutupiwa picha hizo zilizowakera baadhi ya watu si wa Wema, bali ni wa meneja wake, Martin  Kadinda.
 
WIKIENDA LAANZA NA WEMA
Licha ya kutambua hilo, Jumamosi iliyopita, Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka Wema kwa njia ya simu ya kiganjani ili kumuuliza kama ana amani moyoni kufuatia picha zake zilizotafsiriwa kuwa ni za kuinajisi swaumu yake kutumbukizwa mtandaoni, lakini simu yake haikupatikana hewani.
 
Wema katika vazi la hijabu.
KADINDA APATIKANA, HEBU MSIKIE

BOMU JINGINE TENA MKUTANO WA CHADEMA DAR,POLISI WAHUSIKA


 
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana.
-POLISI WATHIBITISHA KULILIPUKA
-LAKINI WADAI NI BAHATI MBAYA
Ikiwa ni takribani mwezi mmoja tu tangu bomu lilipolipuka kwenye mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Arusha, jana tukio kama hilo lilitokea jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, ambao aliutishia kwa lengo la kuwaelezea wananchi mrejesho wa yaliyojiri bungeni hivi karibuni na kuhamasisha wananchi kushiriki kutoa maoni kwenye rasimu ya Katiba mpya.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...