MBUNGE WA KINONDONI NA KASHFA YA MADAWA YA KULEVYA,ATINGA POLISI
KUFUATIA
kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya
nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai
29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Kwa mujibu wa chanzo
chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar
na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa
Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na
kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,”
kimesema chanzo chetu.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi
Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na
kuwataka wamchunguze kwa kina.
“Kila kinapofika kipindi kama hiki
huwa kuna vuguvugu la uchaguzi, hivyo maneno kama haya husemwa ili
kuharibiana sifa, nimewataka polisi wanichunguze na watakachokipata
watoe taarifa kwa wananchi,” alisema.
Hivi karibuni Mbunge huyo
alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na
biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong
kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya
kulevya.
Hata hivyo, Mbunge huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema
kuwa hausiki kwa njia moja ama nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe
jina lake kamili, namba yake ya ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa
nchini ili ukweli ujulikane.
No comments:
Post a Comment