MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa
mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
MCHEZO MZIMA
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na
Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani
City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.
Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya
maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa
wamekaa nje ya mgahawa huo.
Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu,
aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na
mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa
Romy kwa vile alikuwa nayo.
Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha
aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne
katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo
Sinza-Kumekucha, Dar.
WAKUTANA
Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.
Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana
Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari
aina ya Toyota Opa.
WEMA ATAJWA
Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari
la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia
kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema
Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.
Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha
kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu
iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo
atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.
Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.
Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.
‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.
Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye
alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo
alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.
Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo
yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu
80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.
Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu
baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya na walipopanga kukutana mara ya
pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond
alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.
Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe
ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama
atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo,
waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano
yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake
Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu
kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi
alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na
kumpa jina la Rujeina.
SASHA AKIRI
Baada ya kupata madai hayo, gazeti hili lilimsaka Sasha ili
kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri
kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena,
naye aliacha kumfuatilia.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua
yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea
mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile
kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.
HUYU HAPA DIAMOND
Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya
na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza:
“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Katika kuonesha ‘usiriazi’, gazeti hili liliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha.
Source@global publishers