Ismail Aden Rage.
Baada ya Ismail Aden Rage kurudi Tanzania usiku wa Novemba 22, 2013,
akiwa Airport Dar es salaam aliahidi kwamba Novemba 23, 2013
angezungumza na waandishi wa habari kuhusu yote yaliyotokea wakati akiwa
nje ya nchi ikiwemo kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.Mkutano ambao ulikuwa ufanyike saa saba mchana kwenye makao makuu ya Klabu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi umeahirishwa mpaka Novemba 24, hapohapo makao makuu.
"Nimeahirisha mpaka kesho, kwa sasa niko klabuni na wanachama wangu tunapiga stori tu, hakuna neno… napiga stori na wanachama wangu," alikaririwa Rage.
No comments:
Post a Comment