kabesejr blog

kabesejr

albino

Sunday, March 26

Nape Nnauye Aamsha Shangwe Uwanaja wa Taifa Wakati Samatta Akitupia 2

MBUNGE wa Mtama, mkoani Lindi kwa Tiketi ya CCM, Nape Nnauye leo Machi 25, 2017 ameamsha shangwe kwenye Uwanja wa Taifa wakati wa mechi kati ya Taifa Stars na Botswana.
Nape alinyanyuka kuwasalimia mashabiki wa Taifa Stars wakati wa kipindi cha mapumziko kwenye mchezo huo, jambo lililowashangaza wengi na kuanza kumshangilia kwa nguvu huku wakipiga makelele za kuimba Nape… Nape…. Nape!.
Pamoja na kumshangilia, wengi walikuwa wakigongana kutaka kupiga naye picha naye aliwapa nafasi mashabiki hao.


Baadaye Nape alionekana akiwa ameketi na kupiga stori na Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo. Nape ambaye nafasi yake aliteuliwa Mwakyembe juzi Alhamisi, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni.
Katika mechi ya leo, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa bao 2-0 zidi ya Botswana, mabao yote yakifungwa na Straiker wa Kimataifa wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta kunako dakika ya 3 na 87 ya mchezo huo.
Source: GP

Ney Wamitego Akamatwa Morogoro leo Asubuhi

Kutoka Morogoro asubuhi hii Msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni ametoa wimbo mpya anaodai amezungumza ukweli wa moyo wake kwa kinachoendelea, amethibitisha kukamatwa na Polisi.
Nay ameandika kwenye Instagram yake “Nimekamatwa kweli muda huu nikiwa Hoteli Morogoro baada ya kumaliza kazi yangu iliyonileta, napelekwa Movemero Police, Nawapenda Watanzania wote #truth #Wapo”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...