kabesejr blog
kabesejr
albino
Wednesday, June 27
MANENO YA ZITTO KABWE KUTOKANA NA UTEKAJI WA DR ULIMBOKA
Dr. Steven Ulimboka
Dr. Steven Ulimboka
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOINimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
Sources zittokabwe.wordpress.com
DR ULIMBOKA AOKOTWA BAADA YA KUTEKWA
Sasa uchokozi umefikia pabaya na hii sasa ni vita!!
Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.
Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji. (source chanzo cha kuaminika).
UPDATE:
Inaelekea waliomteka si watu wema kabisa, Dr. Ulimboka kaokotwa sehemu akiwa katika hali mbaya sana!
Tuesday, June 26
50 Cent Injured In A Car Accident (Exclusive Pictures)
50 Cent
was in a bad accident tonight as his bullet-proof SUV was rear-ended by
a Mack truck on the LIE in NYC.
He was put on a stretcher and taken to the nearest Queens hospital where they are currently running test on his neck and back.
His driver is also currently in the hospital as the SUV almost flipped over.
He was put on a stretcher and taken to the nearest Queens hospital where they are currently running test on his neck and back.
His driver is also currently in the hospital as the SUV almost flipped over.
The truck driver reportedly told police his loaded shifted
and lost control of the vehicle.
More as it develops..
UPDATE
#1:
added pics of the Mack Truck
added pics of the Mack Truck
Posted by sophia kessy at
6:55 AM
Subscribe to:
Posts (Atom)