kabesejr blog

kabesejr

albino

Tuesday, March 27

BIF KATI YA NIKKI MBISHI NA WEUSI


 Nikki
Weusi
Baada ya Nikki Mbishi kutangaza rasmi kujitoa Lunduno, sasa asanuka na bifu la yeye na Weusi. Nicki Mbishi aliyefanya mahojihano na moja ya redio maarufu hapa bongo amesema, ameshangaa sana kuona Bonta kutangaza bifu nayeye. Kisa cha bifu hilo inasemekana kuwa wanagombania jina la CONSCIOUS ambalo linatumiwa na wasanii hao. Kwa mujibu wa Bonta anasema yeye ndio mwanzilishi wa jina hilo hivyo basi Nicki Mbishi anakopi jina hilo na kulitumia yeye. Mbali na malalamiko hayo yanayohusu jina la CONSCIOUS, Nicki Mbishi pia amelalamikiwa kuwapiga madongo wakali hao kutoka kundi la Weusi mfano, kuna mstari unasema: “iweje Nicki wa pili wakwanza hajulikani” hii inaweka wazi kuwa jamaa amediss Nicki wa pili kujiita hivyo.
Nicki Mbishi amesema “Kwakuwa wameamua kutangaza bifu basi acha liwe bifu kati yangu na hao wanao jiita weusi au waanzilishi wa Hip Hop Tanzania, kwanza hata KalaPina alisema kwenye tamasha la Dar Live kuwa Hip Hipo imeanzia Dar sio A-Town kama wasemavyo wao”.
Bonta amesema “kwakuwa kila mtu anauhuru wa kufanya au kuongea katika hii nchi basi acha awehuru, me sishangai anayosema yeye kwakuwa yuko huru kisheria hivyo muacheni aamue kujiita au kufanya analotaka, ila nachoona anataka kutafuta jina kupitia weusi”.
Kwa mujibu wa weusi na wakali wengine kutoka Lunduno wanasema Nicki Mbishi anaamua kujitafutia jina kwa kuwa anaona ameshapotea kwenye game la Hip Hop ndio maana anajaribu kukopi majina ya watu na kujipa yeye.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...