kabesejr blog

kabesejr

albino

Thursday, March 22

KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA QT 2012

TANGAZO

Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia Watahiniwa wote wa Kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE) mwezi wa Oktoba, 2012 kwamba mwisho wa usajili kwa ada ya kawaida bila faini umesogezwa mbele mpaka 04/03/2012.
Watahiniwa watakaojisajili kuanzia tarehe 05/03/2012 hadi 31/03/2012 watatakiwa kulipa ada ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi tarehe 31/03/2012.
Baraza la Mitihani linasisitiza kuwa hakuna Mtahiniwa atakayesajiliwa baada ya tarehe 31/03/2012. Watahiniwa ambao bado hawajajisajili hadi sasa wanashauriwa kujisajili kabla ya tarehe 05/03/2012 ili kuepuka kulipa ada na faini kwa ajili ya kuchelewa kujisajili.
LIMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...