SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limetaja viingilio vya mechi ya Yanga na Simba
itakayochezwa Jumatano, Oktoba 3 mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kiingilio cha chini kabisa kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani
ambavyo ni 19,648 kwenye Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
60,000.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia kabesejr leo kwamba,
mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja
huo kuanzia saa 11:00 kamili jioni na watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo
wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh.
7,000 kwa tiketi moja.
Wambura
alitaja viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya
chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa
sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji
748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
Kabla ya
mechi hiyo itakayorushwa moja kwa moja na Talevisheni ya Super Sport, leo Simba
wanaonolewa na Mserbia, Profesa Mserbia Milovan Cirkovick wanacheza na Prisons
na kesho Yanga walioleta kocha mpya Mholanzi, Ernie Brandts wanacheza na African
Lyon, mechi zote Uwanja wa Taifa.
Wakati Simba
wamefika kambi visiwani Zanzibar, Yanga wapo hapa hapa Jijini, maeneo ya
Changanyikeni.
source: aishaclassic.blogspot.com