kabesejr blog

kabesejr

albino

Thursday, September 13

KILICHOIKUTA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


Marehemu Daudi Mwangosi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...