Manchester City inatumai kutumia maarifa ya Ofisa wake Mtendaji Mkuu
mpya, Ferran Soriano wa Barcelona kuwanasa mshambuliaji wa thamani ya
juu, Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 21, kiung Sergi Roberto,
mwenye miaka 20 na winga Gerard Deulofeu, mwenye miaka 18.
Emile Heskey - ambaye yuko huru tangu aondoke Aston Villa
mwishoni mwa msimu uliopita, anatakiwa na timu ya Ligi ya Conference,
Macclesfield ambayo inaamini mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool
na England mwenye umri wa miaka 34, atawarejesha kwenye Ligi za Soka
England.
Fulham inamtaka kipa wa Standard Liege, Sinan Bolat, mwenye umri wa miaka 24, akazibe nafasi ya Mark Schwarzer.
Kiungo David Meyler, mwenye umri wa miaka 23, atabaki Sunderland baada ya kocha Martin O'Neill kughairi kumtoa kwa mkopo Hull.
QPR HAITAMSHURTISHA FERDINAND KUMPA MKONO JT
QPR haitamuamrisha beki Anton Ferdinand kupeana mikono na wachezaji wa
Chelsea, licha ya Bodi ya Ligi Kuu kuamua kwamba kanuni za kabla ya
mechi zinabaki kama zilivyo. Ferdinand, mwenye umri wa miaka 27,
ameamua kutofuata itifaki hiyo kwa John Terry, mwenye umri wa miaka 31,
au Ashley Cole, mwenye umri kama huo pia, katika mechi ya kwanza ya
Ligi Kuu dhidi ya Chelsea, tangu Nahodha huyo wa The Blues, Terry
asafishwe na Mahakama kwa kashfa ya ubaguzi dhidi yake.
Mshambuliaji wa Aston
Villa, Darren Bent, mwenye umri wa miaka 28, amesema kwamba hataki
kupuuzia msimu huu, na atathibitisha anastahili kuendelea kuwamo kwenye
kikosi cha England katika zama mpya za kocha Roy Hodgson.
Winga Mnigeria wa Chelsea, Victor Moses alikuwa ana umri wa
miaka 11 wakati wazazi wake wanauawa katika mapambano ya kidini;
"Popote walipo kwa sasa, lazima wajivunie mimi, wanaangalia chini
wakijivunia mimi."
Kocha wa zamani wa Everton, Howard Kendall amemuonya Marouane Fellaini,
mwenye umri wa miaka 24, kuchunga mdomo wake baada ya kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 24, kusema ataondoka Goodison Park Januari.
No comments:
Post a Comment