Kimenuka... Drogba akilindwa na Polisi wakati akitolewa uwanjani. |
Hatari...! Mashabiki wa 'chama' la kina Drogba wakihaha kujiokoa jana baada ya vurugu kuibuka katika mechi yao dhidi ya Senegal. |
Duh...! Kimenuka hadi kitaa.... mashabiki wa Senegal wakikimbia mitaani huku wakiandamwa na mabomu ya machozi baada ya kuzuka kwa vurugu uwanjani jana. |
Yaya Toure (kulia) na wachezaji wenzake wa Ivory Coast wakitolewa uwanjani na 'FFU' wa Senegal baada ya vurugu zilizotokea uwanjani jana. |
Sasa uwanjani hapakaliki tena...! |
Ni vurugu mtindo mmoja baada ya mashabiki wa Senegal kukasirishwa na kipigo cha Ivory Coast dhidi ya timu yao jana. |
Wachezaji Ivory Coast wakitolewa uwanjani. |
Mashabiki wa Ivory Coast wakihaha kujiweka pamoja ili kujiokoa jana. |
Kimenuka mwanaa... hapakaliki tena uwanjani! |
DAKAR, Senegal
Mechi
muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati
ya Senegal na Ivory Coast imefutwa baada ya mashabiki kuvamia uwanja
mjini Dakar juzi.
Mashabiki
wa wenyeji walianza kwa kuwasha moto majukwaani na kurusha mawe na vitu
vingine uwanjani wakati Senegal wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, matokeo
ambayo yangewatoa katika michuano hiyo.
Mashabiki wa Ivory Coast walikimbilia uwanjani kuepuka mashambulizi.
Mashabiki
na wachezaji wa Ivory Coast baadaye walitolewa nje na polisi, ambao
walifyatua mabomu ya machozi kuelekea kwenye majukwaa yaliyofurika
mashabiki.
Taarifa
zimesema kuwa takriban wati 10 -- akiwamo Waziri wa Michezo wa
Senegal,Hadji Malick Gakou -- walijeruhiwa katika vurugu hizo kwenye
Uwanja wa Leopold Sedar Senghor.
Vurugu
hizo zilitokea baada ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba
kufunga goli lake la pili kwa njia ya penati, huku zikiwa zimebaki
dakika 15 kabla mechi kumalizika. Kabla ya goli hilo la penati
lililokuwa la 58 kwake kuifungia Ivory Coast, Drogba alifunga goli la
kwanza katika mechi hiyo kwa njia ya 'fri-kiki'.
Matokeo
hayo yangeiwezesha Ivory Coast kuongoza kwa jumla ya mabao 6-2 baada ya
kushinda pia kwa mabao 4-2 katika mechi yao ya kwanza.
"Vyakula,
vinywaji na chochote kile kilichoweza kurushwa kilirushwa uwanjani,
kutoka katika kona tofauti," Chris Fuglestad, mwanafunzi wa Marekani
anayesoma mjini Dakar, aliiambia BBC.
Shirikisho
la Soka la Afrika (Caf) bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na
tukiuo hilo. Lakini afisa mmoja wa Senegal alikaririwa akisema kwamba
sasa timu yao itafungiwa na Caf.
Wachezaji
ndugu wa Manchester City, Yaya na Kolo Toure walikuwamo katika kikosi
cha Ivory Coast, na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilisema katika
taarifa yake kuwa: "Yaya na Kolo Toure wote wako salama baada ya vurugu
za mashabiki kuvunja mechi wakati Senegal walipoikaribisha Ivory Coast
mjini Dakar."
No comments:
Post a Comment