kabesejr blog

kabesejr

albino

Wednesday, March 28

CHALZ BABA RAIS WA MASHUJAA BAND


Baada ya mwanamuziki chalz baba kuhama kutoka Bend ya Twanga pepeta sasa n rahisi wa bendi yake ya mashujaa.Uchuo uiofanyika tarehe 27 na kumtangaza kwa kshindo kikubwa.

Tuesday, March 27

VIDEO YA SINGLE BOY YA ALLY KIBA & LADY JAYDEE, JIKONI

Hizo ni picha kadhaa zikionyesha kuandaliwa kwa video mpya ya Ali kiba na jaydee.
.
.
.
.

BIF KATI YA NIKKI MBISHI NA WEUSI


 Nikki
Weusi
Baada ya Nikki Mbishi kutangaza rasmi kujitoa Lunduno, sasa asanuka na bifu la yeye na Weusi. Nicki Mbishi aliyefanya mahojihano na moja ya redio maarufu hapa bongo amesema, ameshangaa sana kuona Bonta kutangaza bifu nayeye. Kisa cha bifu hilo inasemekana kuwa wanagombania jina la CONSCIOUS ambalo linatumiwa na wasanii hao. Kwa mujibu wa Bonta anasema yeye ndio mwanzilishi wa jina hilo hivyo basi Nicki Mbishi anakopi jina hilo na kulitumia yeye. Mbali na malalamiko hayo yanayohusu jina la CONSCIOUS, Nicki Mbishi pia amelalamikiwa kuwapiga madongo wakali hao kutoka kundi la Weusi mfano, kuna mstari unasema: “iweje Nicki wa pili wakwanza hajulikani” hii inaweka wazi kuwa jamaa amediss Nicki wa pili kujiita hivyo.
Nicki Mbishi amesema “Kwakuwa wameamua kutangaza bifu basi acha liwe bifu kati yangu na hao wanao jiita weusi au waanzilishi wa Hip Hop Tanzania, kwanza hata KalaPina alisema kwenye tamasha la Dar Live kuwa Hip Hipo imeanzia Dar sio A-Town kama wasemavyo wao”.
Bonta amesema “kwakuwa kila mtu anauhuru wa kufanya au kuongea katika hii nchi basi acha awehuru, me sishangai anayosema yeye kwakuwa yuko huru kisheria hivyo muacheni aamue kujiita au kufanya analotaka, ila nachoona anataka kutafuta jina kupitia weusi”.
Kwa mujibu wa weusi na wakali wengine kutoka Lunduno wanasema Nicki Mbishi anaamua kujitafutia jina kwa kuwa anaona ameshapotea kwenye game la Hip Hop ndio maana anajaribu kukopi majina ya watu na kujipa yeye.

Thursday, March 22

KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA QT 2012

TANGAZO

Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia Watahiniwa wote wa Kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE) mwezi wa Oktoba, 2012 kwamba mwisho wa usajili kwa ada ya kawaida bila faini umesogezwa mbele mpaka 04/03/2012.
Watahiniwa watakaojisajili kuanzia tarehe 05/03/2012 hadi 31/03/2012 watatakiwa kulipa ada ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi tarehe 31/03/2012.
Baraza la Mitihani linasisitiza kuwa hakuna Mtahiniwa atakayesajiliwa baada ya tarehe 31/03/2012. Watahiniwa ambao bado hawajajisajili hadi sasa wanashauriwa kujisajili kabla ya tarehe 05/03/2012 ili kuepuka kulipa ada na faini kwa ajili ya kuchelewa kujisajili.
LIMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...