kabesejr blog

kabesejr

albino

Saturday, July 14

WEMA AVAMIWA NA MAJAMBAZIII?


SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.

KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.

WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo na kuiba vitu mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme ndani ya gari (control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na madirisha (power window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma (side miller).
Vitu vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni ‘makapeti’ ya ndani na vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani ya geti hilo.

WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na uvamizi huo ambao umemfanya kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa akizingatia kuwa tukio hilo limetokea wakati nyumba yake ina walinzi wawili.
“Ni kweli nimeibiwa hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila mazingira ya kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana walinzi wangu wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?” alisema Wema kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea: “Sikuwa na namna kwao, nilikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe utatuzi wa jambo hili sambamba na kuwabananisha walinzi wangu ambao walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini kama geti la kutokea nje lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe. Lakini hili geti ni gumu, mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua masaa matano ambapo kungekuwa kumekucha.”

INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati ya Juni mwaka huu, staa huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, alitangaza kupitia runinga kwamba anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina kila kitu ndani.
Kwa mujibu wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya nyumba hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja wa Wema, Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na samani zake shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.

HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya Jumanne kuzungumzia tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi zilithibitisha Wema kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni majambazi

S0urce global publishers.com

ALIOYEMTEKA DRE ULIMBOKA HUYU HAPA

Mtuhumiwa wa kwanza kwenye ishu ya kutekwa na kuteswa kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dr Ulimboka Steven amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kujisalimisha kwenye kanisa la ufufuo na uzima la Mchungaji Jospephati Gwajima kwa lengo la kuungama dhambi zake.
Baada ya mtuhumiwa huyo ambae ni raia wa Kenya aitwae JOSHWA GITU MUHINDI kwa mujibu wa hati yake ya kusafiria kukamatwa, amekiri kuhusika kumteka na kumtesa Dr Ulimboka akiwa na wenzake 12 waliokodiwa na mtu anaehisi kuwa anatoka serikalini.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa mtu huyo ambae imefahamika ni mwanachama wa kundi la GANGSTAR lenye makazi yake Kenya na linaongozwa na Mtu anaetajwa kwa jina la SILENCER na sasa wanaendelea na uchunguzi zaidi.

MAGAZETI YA LEOO HII CHEKI JINSI SHEREHE YA WASAGAJI ILIVYOFANA DAR

 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Thursday, July 12

Mrembo wa Sinza kupatikana leo (Ijumaa) ukumbi wa Mawela



Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka mrembo wa Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yatafanyika leo (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican City.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia warembo hao wanawania kitita cha shs. 500,000 cha mshindi wa kwanza katika mashindano hayo yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’.
Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, shs 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata shs 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata shs 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Majuto alisema kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo watachuana  ili kumpata mshindi atakayepata shs 50,000 kutoka kwa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na kiingilio kitakuwa shs 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa urembo wa Sinza wasugue kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Warembo wanaowania taji hilo ni Warembo wanaowania  taji hilo ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John,  Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na  Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters,  Lady Pepeta na flexi.

BABA DIAMOND AIBUKA,ANENA MAZITO!!!!



ASAKWA PANDE ZOTE ZA DAR
Awali lilitangulia zoezi la kumsaka baba Diamond katika pande zote za Jiji la Dar es Salaam ili kumsikia alichonacho moyoni kuhusu mafanikio ya mwanaye huku taarifa za mahali anapoishi zikipotoshwa na watoa habari wetu.
Wapo waliosema mzee huyo anaishi Kibamba, wengine Mbagala, pia wapo waliodai anakaa Manzese au Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Timu ya mapaparazi wa Amani ilizama kazini kikamilifu ikiapa kumnasa mzazi huyo popote alipo na hatimaye Julai 2, 2012 saa saba mchana ilifanikiwa kupabamba nyumbani kwake, Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam lakini mwenyewe hakuwepo.
Ziliachwa salamu za utambulisho kwa jirani mmoja ili atakaporudi mzee huyo amtaarifu kuwa mapaparazi watarudi siku nyingine.
Julai 7, 2012 saa tano asubuhi mapaparazi wetu walitinga nyumbani hapo na kumkuta mzee huyo akisema alipata salamu na alikuwa akisubiri ujio huo, hivyo akawa amejiibua mwenyewe.

AANZA KWA KUANIKA HISTORIA KWA UFUPI
Baada ya salamu na utambulisho, mzee huyo alianza kwa kukiri kwamba kweli yeye ni baba mzazi wa Nasibu (Diamond) na kuweka wazi kwamba aliachana na mama mzazi wa msanii huyo miaka 9 iliyopita.
“Ni kweli mimi ndiye Abdul Juma, ni baba mzazi wa Nasibu au Diamond. Eee, mimi niliachana na mama Nasibu miaka tisa iliyopita, tena siku tunatengana niliondoka nyumbani saa tisa usiku, maana nilikuwa naishi kwao (ukweni).
AMGEUKIA DIAMOND
Kinyume na matarajio ya kuzungumzia mafanikio ya mwanaye kwa sasa, baada ya kuwekwa katikati na waandishi wetu, mzee Abdul ‘aliangusha’ kilio cha lawama kwa Diamond kuhusu matendo anayomfanyia kila kukicha.
Mzee huyo anayeonekana ‘kisharobaro’ alisema mafanikio makubwa aliyonayo mwanaye yasimfanye ashindwe kumthamini yeye kama baba na mapenzi yake kuyaelekeza kwa mama yake tu.
“Kuhusu Diamond, labda nimwambie huyu mtoto kuwa, amepata mafanikio ndiyo, lakini mafanikio hayo yasimfanye ashindwe kunithamini mimi kama baba yake na kupeleka mapenzi yote kwa mama yake tu,” alisema.
NI KWANINI?
“Nasema hivyo kwa sababu, zamani kabla jina lake halijawa kubwa, mawasiliano yetu yalikuwa mazuri sana, lakini nikaja kushangaa baada ya kuwa staa, akakata mawasiliano na mimi baba yake, aliangalie hilo.”
Akaongeza: “Sisemi kwa sababu nataka awe ananiletea hizo fedha zake, la hasha! Ila mimi kama baba yake ajue kuniheshimu.
“Diamond nampigia simu hapokei, namtumia meseji hajibu, maana yake nini? Naumizwa sana na kitendo cha kutopokea simu yangu kila ninapompigia kumjulia hali. Na hali hii ameanza mara baada ya kupata mafanikio.
JARIBIO LAIVU Katika kuthibitisha hilo, paparazi wetu alimtaka mzee huyo kumwendea hewani mwanaye ili kujiridhisha kama kweli ‘hapokeagi’ simu yake, simu ikapigwa, ikaita wee mpaka ikakatika.
Baba Diamond: “Si umeona, si nilikwambia ukawa huamini.”
MARA YA MWISHO KUMUONA DIAMOND
Mzee huyo aliendelea kutiririka kuwa, mara ya mwisho Diamond kufika nyumbani kwake ilikuwa mwezi wa tatu (Machi) mwaka huu baada ya hapo mawasiliano yakakatika.
“Diamond alikuja nyumbani kwangu mwezi wa tatu ikiwa ni mfungo wa tatu katika dini yetu ya Kiislam, akanipa fedha. Baada ya hapo hatujaonana tena wala hanijulii hali,” alilalama mzee wa watu.
SMS YA MWISHO KUIJIBU
Alisema Aprili, mwaka huu, Diamond alipotwaa tuzo tatu za Kili Music Awards 2012, yeye alimtumia ujumbe mfupi wa maneno akimpa hongera naye akajibu asante baba. Lakini baada ya hapo ikawa imetoka.
“Baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo za Kili, mwaka huu nilimpigia simu mwanangu ili nimpongeze, hakupokea, nikamtumia SMS ndipo akajibu, ‘asante baba’, mchezo ukaishia hapo.
“Namshukuru sana dada yake, Mwajuma Abdul (Queen Darleen) yeye ndiyo yupo karibu sana na mimi kwani mara kwa mara anakuja kunitembelea na wakati mwingine hunikumbuka kwa fedha, hata pale aliposhinda tuzo ya Wimbo Bora wa Dancehall alifika nyumbani kunionesha tuzo yake, binafsi nilijisikia furaha,” alisema mzee Abdul ambaye kwa sasa hana mke.
HAJUI ANAPOISHI MWANAYE
Mbali na msanii huyo kutopokea simu ya baba yake kila anapompigia, vile vile mzee huyo alidai hajamuonesha wapi anapoishi.
“Huyu mtoto hajawahi kunionesha anapoishi, sijui anafikiri nikiwa karibu naye nitakuwa namuomba fedha. Mimi sina njaa ‘kihivyo’ na wala sitaki fedha zake, ila ninachotaka salamu tu, nasikiasikia anaishi Mwenge (usahihi ni Sinza Mori) lakini hataki kunionesha.
“Ninachojua yote haya yana mwisho kwani nyota aliyonayo sasa kuna siku itazima. Simuombei mabaya lakini inaniuma sana kunifanyia hivyo.”
DIAMOND APIGIWA SIMU MARA KUMI NA MBILI
Baada ya kupata matamshi hayo ya baba mzazi wa Diamond, mwandishi wetu siku ya Jumanne alifanya jitihada za kumpata msanii huyo ili ajibu ‘mashitaka’ hayo lakini licha ya kupigiwa simu mara kumi na mbili hakupokea.
Mbali na kupigiwa simu, paparazi wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi, lakini pia hakujibu kitu. Juhudi za kumsaka zinaendelea.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...