Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya kumsaka mrembo wa Sinza, Redds Miss
Sinza 2012 yatafanyika leo (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten
Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican City.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha
Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia warembo hao wanawania kitita
cha shs. 500,000 cha mshindi wa kwanza katika mashindano hayo yatakayopambwa na
bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’.
Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy
Entertainment, Majuto Omary alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa
mshindi wa pili, shs 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi wa nne na wa tano
watapata shs 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata shs 100,000 kila mmoja
kama kifuta jasho.
Majuto alisema kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’
kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo
watachuana ili kumpata mshindi
atakayepata shs 50,000 kutoka kwa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na kiingilio kitakuwa shs
10,000 kwa viti vya kawaida na shs 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo
fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa urembo wa Sinza wasugue kisigino
na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Warembo wanaowania taji hilo ni Warembo
wanaowania taji hilo ni Mariam Miraji,
Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said,
Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold,
Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com, Brake
Point, Fredito Entertainment, Screen Masters, Lady Pepeta na flexi.
No comments:
Post a Comment