Mtuhumiwa wa kwanza kwenye ishu ya kutekwa na kuteswa kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dr Ulimboka Steven amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kujisalimisha kwenye kanisa la ufufuo na uzima la Mchungaji Jospephati Gwajima kwa lengo la kuungama dhambi zake.
Baada ya mtuhumiwa huyo ambae ni raia wa Kenya aitwae JOSHWA GITU MUHINDI kwa mujibu wa hati yake ya kusafiria kukamatwa, amekiri kuhusika kumteka na kumtesa Dr Ulimboka akiwa na wenzake 12 waliokodiwa na mtu anaehisi kuwa anatoka serikalini.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa mtu huyo ambae imefahamika ni mwanachama wa kundi la GANGSTAR lenye makazi yake Kenya na linaongozwa na Mtu anaetajwa kwa jina la SILENCER na sasa wanaendelea na uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment