kabesejr blog

kabesejr

albino

Saturday, May 16

AMISOM YAFELISHA SHAMBULIO LA AL-SHABAB, SOMALIA



Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM.
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM wametangaza kuwa, wamefanikiwa kufelisha shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab nchini humo.

Askali hao wakiwa kwenye oparesheni hiyo.
Taarifa iliyotangazwa na Sam Kavuma, mmoja makamanda wa askari hao, imesema kuwa wanamgambpo wa al -Shabab walijaribu kudhibiti kambi za kijeshi za serikali katika eneo la Shabili Sufla la kusini mwa Somalia, lakini askari wa Amisom wamezima shambulio hilo.
Kavuma ameisifu operesheni hiyo aliyoitaja kuwa iliyofanikiwa na kuongeza kuwa, kundi la al -Shabab limefeli vibaya katika jaribio hilo na kwamba wamekimbia baada ya vikosi hivyo kuwasili eneo la tukio. Kamanda huyo wa AMISOM ameongeza kuwa kundi la al -Shabab linapanga mashambulizi ya kudhibiti kambi za kijeshi ili kurejesha nguvu yao iliyodhoofika sana.
Hayo yanajiri katika hali ambayo duru za habari zimeripoti kwamba kundi hilo la kigaidi lilikuwa limedhibiti baadhi ya maeneo ya kusini mwa Somalia.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...