kabesejr blog

kabesejr

albino

Saturday, May 16

MAREKANI YAFUNGA UBALOZI WAKE MJINI BUJUMBURA-BURUNDI


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Jeff Rathke.
Serikali ya Marekani kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje imetangaza kufunga ubalozi wake wa mjini Bujumbura, Burundi kutokana na kuendelea machafuko nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na ubalozi huo imesema kuwa, Marekani imeamua kufunga ubalozi wake huo kutokana na kuendelea machafuko yanayohatarisha usalama.
Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Jeff Rathke ubalozi huo utaendelea kutoa huduma za dharura kwa raia wake katika kipindi cha kufungwa kwake huko Burundi.
Jeff amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, inawataka raia wake kuacha kuelekea nchini humo, huku wale waishio Burundi wakitakiwa kuondoka haraka iwezekanavyo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kufeli jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Pierre Nkurunziza, baada ya kujiri machafuko ya wiki mbili, suala ambalo linatafsiriwa na weledi wa mambo kuwa linazidisha uwezekano wa kuibuka machafuko makali ndani ya taifa hilo dogo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuendelea maandamano ya wapinzani wa serikali wanaopinga rais huyo kugombea katika uchaguzi mkuu ujao, nako kunazidi kuifanya tete hali ya mambo nchini Burundi.
Hadi sasa watu kadhaa wamekwishauawa katika vurugu hizo na zaidi ya laki moja kuwa wakimbizi katika nchi za Tanzania, Rwanda na Uganda.
CREDIT: IRAN SWAHILI

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...