Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael
Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti
katika kilabu ya Real Madrid.
Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii.Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa hakuna makubaliano yalioafikiwa.
Klabu ya West Ham pia iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifunza Chelsea na Liverpool.
Mkufunzi wa West Ham ambaye anaiandaa West Ham dhidi ya Newcastle anatarajiwa kuanzisha mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake wiki ijayo.
Benitez alianza kazi ya ukufunzi katika kilabu ya Real Madrid B na pia amewahi kuifunza Valladolid,Osasuna,Etramadura,TenerifeValencia na Inter Milan.
No comments:
Post a Comment