Kikao kikiwa kinaendelea jana usiku.
Mwenyekiti
wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Bw. Mugwengezo Chauvineau
akiongea na waandishi wa habari Serena Hotel Dar jana usiku .
Dkt.
Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika
harakati za usawa nchini Burundi, akiongea na waandishi wa habari jana
usiku.
Mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi kwa mara ya
kwanza amefika nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia mkutano wa dharula
kati ya viongozi watano wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu nchi
ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyepo
madarakani kutaka kuongeza muda wake.
Akiongea na waandishi wa habari usiku kuamkia leo, Mkuu huyo wa
vuguvugu la maandamano ya Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na
Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria na katiba
hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea
kupinga Rais kuendelea kuwania kwa muhura wa tatu.
Amezungumzia juu ya waandamanaji baada ya wiki tatu bado wapo
barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa
sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru
waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza
kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji
wa mambo ambayo yamezungumziwa.
Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi
ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate
kurejea nchini kwao.
Pia ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali
inayoendelea kwa sasa Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani
imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi
iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo
ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.
Kuhusu jaribio la mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo
Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi, kiongozi huyo
amaesema kwamba ni kuongezea muhula wakati tayari alisha tawala kwa
miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi,
hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa muhula wake ni
muhura baki na haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi
pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu
zisinge kuwepo.
Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula
mitatu. Pia Warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena
damu inamwagika.
Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.
Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa
amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea
kuwa madarakani kwa awamu ya tatu.
CHANZO: BLOG ZA MIKOA
No comments:
Post a Comment