Stori ni kwamba msanii
wa Bongo fleva Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari Morogoro road
ambapo kwa mujibu wa djchoka.blogspot.com ni kwamba tairi la mbele
lilipopasuka na gari likaacha njia na kugongana uso kwa uso na fuso
ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha
Roma kurudi lilipotokea.
Roma amemuambia Dj Choka
kwamba anaelekea hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye
gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.
Roma amepata ajali hii
leo ikiwa ni siku 18 tu toka msanii mwingine wa bongofleva Chege kupata
ajali ya gari yake kwa kumgonga mtu wa pikipiki alieingia barabarani
ghafla na kusababisha gari kuharibika.
No comments:
Post a Comment