kabesejr blog

kabesejr

albino

Friday, August 3

MRISHO NGASA KUANZA MAZOEZI NA SIMBA, NA HILI NDIO GARI ALILOPEWA PIA.


Hili ndio gari jipya la Mrisho Ngasa alilopewa kwenye huo uhamisho wa kuingia Simba kwa mkopo akiwa anaingia nalo kwenye mazoezi na Simba leo.
Mrisho Ngasa ni baba wa watoto watatu katika ndoa aliyofunga miaka minne iliyopita.
Ngasa akiwa anaingia kwenye mazoezi Coco beach na club yake mpya ya Simba.
Leo ndio Mrisho Ngasa ameanza mazoezi na Simba leo.
.
Salute kwa Saleh Ally wa gazeti la Champion kwa kunitumia hizi picha.
Jinsi Mrisho Ngasa alivyopokewa na mashabiki wa Simba kwenye makao makuu ya club hiyo.
Jana Club ya soka ya Azam ilitangaza kwamba Mchezaji wao Mrisho Ngasa tayari amepelekwa Simba kwa mkopo ambapo Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) kwa mwezi pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba.
Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki Azam Fc, Pia iliwekwa wazi kwamba Azam haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa, Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC.
Azam ilisema “Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu, Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu”
Azam ilisema kosa alilolifanya Ngasa ni kubusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati bado ni mchezaji wa Azam hivyo ilionekana ni kitendo cha nidhamu mbovu na kuidhalilisha brand ya Azam.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...