kabesejr blog

kabesejr

albino

Saturday, August 4

YANGA WAPELEKA KOMBE BUNGENI, MAMA KARUME KUMUAPISHA MANJI KESHO

Yanga watapeleka Kombe Bungeni Jumatatu



Na Prince Akbar
MAMBO mawili zaidi makubwa Yanga, ukiacha suala la Said Bahanuzi na Didier Kavumbangu, kesho majira ya saa 4:00 asubuhi, uongozi mpya wa Yanga ‘utaapishwa’ na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Mama Fatuma Karume, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Baada ya hapo, Wachezaji na viongozi wa Yanga watasafiri kwenda Dodoma, kwa ajili ya mwaliko wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wapenzi wa klabu hiyo, Jumatatu.
Wabunge hao, wamewaalika wachezaji wa Yanga, baada ya kutwaa taji la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Jumamosi iliyopita, wakiifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye fainali, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Julai 15, mwaka huu, Yanga ilipata viongozi wapya, ambao ni Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji, Abdallah Bin Kleb, George Manyama na Mussa Katabaro.
Hao wanaungana na Wajumbe wengine waliosalia kutoka uongozi uliochaguliwa mwaka juzi, Mohamed Bhinda, Titto Osoro, Salim Rupia na Sarah Ramadhan, baada ya wajumbe wengine, wakiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu.    
Source binzubeiry.blogspot.com

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...