Bolton
itampa ofa ya kuendelea kubaki klabuni Fabrice Muamba katika nafasi
nyingine, baada ya kiungo huyo kulazimika kustaafu soka, miezi mitano
baada ya kupoteza fahamu uwanjani kwa tatizo la moyo.
Uamuzi
huo ulichukuliwa baada ya Muamba kuonana na mtaalamu bingwa wa matatizo
ya moyo, Pedro Brugada nchini Ubelgiji wiki iliyopita. Pamoja na hayo,
upasiaji wa kusafisha moyo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24
ulikwenda vizuri.
Bolton's Fabrice Muamba alipata mataizo ya moyo Machi, mwaka huu
Muamba (katikati) akiwa na famili ya klabu katika siku ya kufurahia, Jumapili
Muamba akiwa amebeba Mwenge wa Olimpiki Waltham Forest
Muamba alipata matatizo ya moyo Uwanja wa White Hart Lane mwezi Machi
Wachezaji wa Bolton na Spurs na kocha wa Wanderers, Owen Coyle (katikati),wakimuangali Muamba akipatiwa huduma ya kwanza
Meseji
kibao za kumtakia kupona haraka Muamba zikiwa zimewekwa katika Uwanja wa
Bolton, Uwanja wa Reebok, wakati alipokuwa hospitali
Dunia ya soka iliungana kumtumia ujumbe wa kumuombea kupona mapemaMuamba
Muamba na
mtaalamu wa moyo, Dk Andrew Deaner (kushoto) na Mshauri wa masuala ya
moyo, Dk Sam Mohiddin, madaktari ambao waliokoa maisha yake
Muamba akitoa machozi aliporejea kwenye Uwanja wa Reebok, Mei mwaka huu
Muamba akifuta machozi Uwanja wa Reebok, Mei mwaka huu
Muamba na mpenzi wake Shauna baada ya kupona
Muamba alipewa Shahada ya heshima Chuo Kikuu cha Bolton
Fabrice Muamba: Kutoka Kinshasa hadi Ligi Kuu England
1988: Alizaliwa April 6 mjini Kinshasa, Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).
1999: Alikwenda England akiwa ana umri wa miaka 11, kuungana tena na baba yake ambaye alikimbia vita Kongo.
2002:
Alijiunga na timu ya vijana iliyoundwa na Arsenal - klabu ambayo
alikuwa anaishabikia alipokuwa mdogo nyumbani kwao - kabla ya kuhitimu
katika Akademi hiyo miaka miwili baadaye.
2005:
Alisaini mkataba na Arsenal na kucheza mechi mbili za kikosi cha kwanza
zote zikiwa za Kombe la Ligi dhidi ya Sunderland, Oktoba 25.
2006:
Agosti alijiunga na Birmingham kwa mkopo wa muda mrefu na huko alicheza
mechi 36 kabla ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa msimu.
2007: Me 11 - Alihamishiwa moja kwa Birmingham baada ya klabu hiyo kukubali kulipa pauni Milioni 4 Arsenal.
Agosti
21 - baada ya kuchezea timu zote za vijana za England kuanzia U-16s,
Muamba alichezeshwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha England U-21
dhidi ya Romania, mechi ya kirafiki.
2008: Juni - Scores alifunga mabao mawili katika mechi 37 za ligi msimu wa 2007/08, lakini hakuinusuru Birmingham kushuka.
Agosti 7 - Alisaini Bolton baada ya Trotters kukubaliana dau la pauni Milioni 5 na Birmingham kwa ajili ya kiungo huyo.
2010: Agosti 10 - Alisaini mkataba mpya wa miaka minne Bolton, ambao ungemalizika mwaka 2014.
2011: Juni - aliichezea England U-21 katika michuano ya Mataifa ya Ulaya nchini Denmark.
Agosti 13 - alifunga bao lake la tatu katika ligi akiwa na Bolton ikiifunga 4-0 QPR.
Agosti 13 - alifunga bao lake la tatu katika ligi akiwa na Bolton ikiifunga 4-0 QPR.
2012:
Machi 17 - Muamba alizimia uwanjani dakika ya 41, Bolton ikicheza
mechi ya Kombe la FA naTottenham Uwanja wa White Hart Line, kabla ya
kupelekwa katika hospitali ya London Chest, ambako alitibiwa hadi
kupona.
Agosti 15 - Anatangaza rasmi kustaafu soka, baada ya kushauriwa na daktari.
No comments:
Post a Comment