Club ya soka ya Yanga
imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji 28 kwa shirikisho la soka
nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa
kuanza mapema septemba mosi.
Katibu mkuu wa Young Africans
Mwesigwa Selestine amesema wamepeleka majina ya wachezaji wote 28 kwa
ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, na hii ni kutokana na benchi la ufundi
kuridhia kuwatumia wachezaji wote.
Kwenye huo usajili
uliowasilishwa August 15 2012, umeambatana na usajili wa wachezaji wa
timu ya vijana U-20 ambapo majina ya wachezaji mahiri wa timu ya Taifa
Saimon Msuva na Frank Domayo.
Usajili kamili kwa timu ya
wakubwa ni kama ifuatavyo: Walinda Mlango ni Yaw Berko, Ally Mustafa
‘Barthez’ na Said Mohamed, walinzi wa pemebeni ni Shadrack Nsajigwa,
Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano
Mwasika, walinzi wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Mbuyu
Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo, viungo wa ulinzi Athuman Idd
‘Chuji’, Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni ni Nizar
Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme, viungo washambuliaji
Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari, washambuliaji Said
Bhanaunzi, Hamis Kiiza ‘Diego’, Didier Kavambagu na Jeryson Tegete, hiyo
ni kwa upande wa timu ya wakubwa.
Kikosi cha wachezaji chini ya
umri wa miaka 20 kina jumla ya majina 22 ambayo ni Geofrey Nyalusi na
Yusuf Abdul kama makipa, walinzi ni Said Manduta, Zuberi Juma, Said
Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said, viungo: Frank Domayo,
Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah,
washambuliaji wa pembeni ni Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah
Salum, Rehani Kibingu, wWashambuliaji: Saimon Msuva, George Banda,
Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo
No comments:
Post a Comment