kabesejr blog
kabesejr
albino
Tuesday, July 24
ANCINI AKUBALI YAISHE KWA VAN PERSIE, AWALAUMU MABOSI WAKE
Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya
MANCINI AKUBALI YAISHE KWA VAN PERSIE, AWALAUMU MABOSI WAKE
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini ana wasiwasi amepoteza mipango katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28.
NA Mancini amekasirishwa na mabosi wa City kwa kutompa ushirikiano wa kutosha katika mpango wa kumsajili Van Persie.
VIGOGO wa Serie A, AC Milan wameanza mazungumzo na mshambuliaji
wa Arsenal, Nicklas Bendtner katika mpango wao wa kumuhamishia Mdenmark
huyo Italia.
KLABU ya Manchester United ya England inamuwania kiungo wa River Plate
ya Argentina, Ezequiel Cirigliano, mwenye umri wa miaka 20, ambaye
anatakiwa pia na klabu za Manchester City ya England na Paris
Saint-Germain ya Ufaransa.
MSHAMBULIAJI anayeondoka Manchester United, Dimitar Berbatov,
mwenye umri wa miaka 31, anaweza kutimkia Urusi, baada ya Zenit St
Petersburg kuonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.
KLABU ya Bayern Munich inajiandaa kumsajili kiungo wa Manchester City,
Nigel de Jong, mwenye umri wa miaka 27, baada ya mpango wa klabu hiyo ya
Ujerumani kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Hispania, Javi Martinez
kama kuzimika hivi.
KLABU ya Tottenham imejiunga kwenye mbio za kumsajili mchezaji
wa zamani wa Liverpool, ambaye kwa sasa anachezea Hoffenheim, Ryan
Babel, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anawaniwa pia na Swansea na
Newcastle.
KLABU ya Fulham anayo pia inaripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili Mholanzi, Babel.
KLABU ya Liverpool inajiandaa kukata dau la pauni Milioni 10
kumsajili mshambuliaji wa Swansea, Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22.
KLABU ya Zenit St Petersburg imejiunga kwenye mbio za kumsajili beki wa
Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, na Manchester City na
Napoli pia zinamtaka.
KLABU ya Nottingham Forest inataka kumsajili Jermaine Jenas,
mwenye umri wa miaka 29, arejee City Ground ambao wanataka kumchukua
kiungo huyo Tottenham.
PARKER KISU TENA
NYOTA Scott Parker anatarajiwa kuikosa mechi ya kirafiki ya
England na Italia mwezi ujao kutokana na kiungo huyo wa Tottenham
kujiandaa kufanyiwa upasuaji ambao akose mechi kadhaa za mwanzoni za
Ligi Kuu
COASTAL UNION YASAJILI MTOTO WA MAXIMO
Monday, July 23
NJIA MPYA MGAMBO KWA WANAOFUNGA MAGARI MJINI
HUYU JAMAA ALIKUA AMEPAK SEHEM AMBAYO HAIRUHUSIWI KU PAK AKAKUTA POLISI
WAMESHA FUNGA TAIRI LAKE ALICHOFANYA AMEFUNGUA NA KUWEKA LINGINE POLISI
WALIPO RUDI WAKAKUTA AMESHAONDOKA
NAHISI INAWEZA ANZA TUMIKA HATA BONGO JIPANGENI POLISI
Subscribe to:
Posts (Atom)