Na Desi
MABINGWA watetezi wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga SC leo wanashuka Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na timu ya Jeshi la Rwanda, APR katika mchezo
wa mwisho wa Kundi C kutafuta mpangilio wa nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu
kwenye kundi hilo.
Yanga yenye pointi tatu,
katika nafasi ya tatu, inaweza kumaliza mechi za kundi hilo katika nafasi ya
pili, iwapo itashinda mechi ya leo, lakini sare au kufungwa itabaki katika
nafasi hiyo hiyo.
APR
yenye pointi nne, inaweza kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye kundi hilo na
kuongoza kwa wastani wa mabao, iwapo itaifunga Yanga, kwani hadi sasa timu hiyo
ya jeshi la Kagame, inalingana kwa wastani wa mabao (GD) na vinara wa kundi
hilo, Atletico ya Burundi, saba kila timu.
Katika mchezo wa leo, Yanga
iko hatarini kuwakosa nyota wake wawili, kipa wake namba moja, Mghana Yaw Berko,
ambaye ni majeruhi sawa na kiungo wa zamani wa APR, Haruna Niyonzima, wakati
kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ yuko fiti kwa asilimia 100 sawa na beki Juma Abdul
aliyeumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Atletico, timu yake ikilambwa 2-0.
Safu ya ushambuliaji ya APR
inaweza kuongozwa na wakali wawili, Mrundi Suleiman Ndikumana na Olivier
Karekezi ambao wote wana miili mikubwa ni hatari kweli sambamba na kiungo
mshambuliaji, Mganda Danny Wagaluka, wakati Yanga bila shaka Said Bahanuzi na
Hamisi Kiiza wataendelea kumpumzisha kwenye benchi Jerry Tegete na Nizar Khalfan
ataongoza safu ya kiungo.
Kihistoria mechi kati ya Yanga
na APR huwa ni kali na za kusisimua tangu zianze kukutana mwaka 1995 katika
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati na mara nyingi watoto wa Jangwani
hunyanyaswa na timu hiyo ya jeshi la Rwanda.
Mechi hiyo itatanguliwa na
mchezo wa Kundi A, kati ya Ports ya Djibouti na URA ya Uganda.
JE
WAJUA?
<!--[if !supportLists]-->1.
<!--[endif]-->Klabu ya Armee Patriotique Rwandaise, maarufu kama A.P.R.,
ilianzishwa mwaka 1993 na inamilikiwa na Jeshi la Rwanda na katika kipindi cha
uhai wake, mafanikio yake makubwa ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda mara
12 (1995, 1996, 1999, 2000, 2001, 2003, 2005, 2006, 2007, 2009, 2010 na 2011),
Kombe la Kagame mara mbili (2004 na 2007) na kufika Nusu Fainali ya Kombe la
Washindi mwaka 2003.
<!--[if !supportLists]-->2.
<!--[endif]-->Young Africans SC maarufu kama Yanga iliyoanzishwa rasmi
mwaka 1935, hadi sasa mafanikio yake makubwa ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya
Bara mara 23, (1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989,
1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009 na 2011), Kombe
la Kagame mara nne (1975, 1993, 1999 na 2011), kufika Robo Fainali ya Klabu
Bingwa Afrika mara tatu (1969, 1970 na 1998) na Kombe la Washindi
1996.
<!--[if !supportLists]-->3.
<!--[endif]-->Wakati Yanga, kocha wake ni Mbelgiji Tom Saintfiet, APR
inafundishwa na kocha Mholanzi, Ernie Brandts- na wakati Yanga Mwenyekiti wake
ni mfanyabiashara milionea, Yussuf Manji, APR Mwenyekiti wake ni mdogo wa rais
wa Rwanda, Paul Kagame aitwaye Alex Kagame.
<!--[if !supportLists]-->4.
<!--[endif]-->Nembo ya Yanga ina alama ya Mwenge, ramani ya Afrika na
mpira- ikimaanisha kushiriki harakati za Uhuru wa Tanganyika, ambayo baadaye
iliungana na Zanzibar na kuwa Tanzania (Mwenge), timu halisi ya Afrika (ramani)
na timu ya mpira (mpira), wakati nembo ya APR ina alama ya mnyama Simba na
mpira- vikimaanisha, ni wafalme kama mnyama Simba porini (Simba) na timu ya
mpira (mpira).
<!--[if !supportLists]-->5.
<!--[endif]-->Wakati Yanga huvalia jezi za rangi ya kijani na njano, APR
wao huvalia jezi za rangi nyeupe na nyeusi siku zote, mara nyingi zikiwa za
mistari ya punda milia.
<!--[if !supportLists]-->6.
<!--[endif]-->Wakati wapinzani wa jadi wa Yanga, nchini Tanzania ni Simba
SC kwa APR wapinzani wao wa jadi Rwanda ni Rayon Sport.
No comments:
Post a Comment