Ray nae ndani
MECHI maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie sasa itachezwa kesho (Mei 5 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo, imerudishwa
nyuma kwa siku moja kupisha mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa
Jumapili.
Mechi
hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni ambapo
viingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh. 2,000, VIP C na B
itakuwa sh. 5,000 wakati VIP A ni sh. 10,000.
Twiga
Stars ambayo kwa sasa haina mdhamini na kambini katika kambi ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani kujiandaa kwa mechi ya mashindano ya Afrika kwa
Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia.
Timu
hizo zitapambana Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa na kurudiana Juni 16 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi atashiriki fainali za AWC
zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment