Hatimaye baada ya
masaa manne ya kusafiri kutoka Khartoom mpaka Shandy wawikilishi wa Tanzania
katika michuano ya kimataifa ya soka Simba SC imefika mjini Shandy salama
kabisa.
Lakini katika hali ya kushangaza wenyeji wao timu Al Ahly Shady wamepotea na kuwaacha wageni wao Simba katika hali tata - kwa mujibu wa mchezaji Emmanuel Okwi wamefikia sehemu mbaya na tangu wamefika takribani masaa sita yaliyopita hawajitia kitu chochote mdomoni. "Bwana huku tumefika lakini kwa shida sana, tunashukuru mungu tumefika salama ila tangu tumefika hapa hatujatia kitu chochote mdomoni na wenyeji wetu hawaonekani. Ila tunawaomba wanasimba na watanzania kwa ujumla waendele kutakia kheri na tunawahidi hizi hila za wasudani hazitowaepusha na kipigo siku ya mechi." - Emmanuel Okwi
No comments:
Post a Comment