MSHAMBULIAJI Robin van
Persie anaweza kulazimishwa kumalizia mkataba wa mwaka mmoja Arsenal, iwapo
atakatakaa mpango wa kusaini mkataba mpya Kikao cha kujadili suala lake
kinafanyika leo nyumbani kwa Wenger.
Wakala
wa Van Persie amesema alifanya majadilioano na Juventus juu ya mkataba wa miaka
minne wenye thamani ya pauni Milioni 6 kwa msimu kwa ajili ya mshambuliaji huyo
wa Arsenal.
KLABU
za Manchester United, Arsenal na Newcastle zinamuwania beki Mfaransa, Mapou
Yanga-Mbiwa mwenye umri wa miaka 22, kutoka Montpellier.
BARCELONA YAMTAKA DROGBA
KLABU
ya Barcelona inafikiria kumchukua mshambuliaji mkongwe aliyemaliza mkataba wake,
Didier Drogba mwenye umri wa miaka 34 kutoka Chelsea.
KLABU
za Arsenal, Tottenham na QPR zinataka kumchukua mkongwe wa Italia, Alessandro
Del Piero mwenye umri wa miaka 37, zikisema atapenda nafasi ya kucheza England
baada ya kuachia ngazi Juventus.
KOCHA
wa Sunderland, Martin O'Neill anataka kumsajili mshambuliaji wa Wolves, Steven
Fletcher na beki wa Chelsea, Ryan Bertrand.
GARY NEVILLE ATAKA YOSSO KIKOSINI
KOCHA
mpya wa England, Gary Neville amemtaka kocha Mkuu wa timu hiyo, Roy Hodgson
kuwapa nafasi wachezaji chipukizi katika Fainali za Euro 2012.
NAHODHA
wa QPR, Joey Barton anafikiria kumtumia wakili wake binafsi, Mel Stein kupambana
na adhabu ya kufungiwa mechi 12 kwa makosa mawili ya vurugu, baada ya kupewa
kadi nyekundu kwenye mechi na Manchester City.
KOCHA
wa Liverpool, Kenny Dalglish amekataa wazo la kuachia ukocha wa timu hiyo ili
apewe majukumu mengine katika mazungumzo na wamiliki wa klabu hiyo, ambayo
vyanzo vinasema hayakwenda vizuri.
LIGI
Kuu ya England inatarajiwa kuanza kutumia teknolojia kwenye lango katikati ya
msimu ujao.
No comments:
Post a Comment