WAREMBO 14 wanataraji kupanda jukwaani Mei 5 mwaka huu,
katika Ukumbi wa Wenge Garden ulipo Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam
kuwania taji la Redds Miss Ukonga 2012.
Akizungumza na Blogu hii mratibu wa Shindano hilo Daudi
Mambya amesema kuwa warembo wote hao 14 wapo tayari kwa kuchuana vikali siku
hiyo na maandalizi kwaajili ya shindano hilo yanaenda vizuri.
“Warembo wote wapo kamili na tayari wako na ari kubwa ya kushindana
jumamosi hii, na hadi sasa hakuna mrembo ambaye anatatizo”, amesema Mambya.
Aidha Mambya amesema awali warembo hao ilikuwa wachujwe na
kubaki 12 lakini kutokana na warembo wote kuwa na vigezo wameamua kuwaacha ili
kuleta ushindani zaidi siku ya mashindano.
Warembo hao ambao watapanda jukwaani kwa show kali na yaaina
yake ya ufunguzi mwaka huu katika majukwaa ya Urembo nchini wataongozwa na
Burudani kali kutoka kwa Mapacha 3.
Mbali na kundi hilo la Mapacha 3 ambalo linawika Jijini Dar
es Salaam kutokana na uhodari wao pia kutakuwepo na burudani nyingine za
wasanii wa kizazi kipya.
Mambya aliwataja warembo hao 14 watakao panda jukwaani kuwa
ni Shekha Shally, Zainab Matagi, Mageshi Boniface, Juliana Henry, Mary Chizi,
Leah John’s na Magdalena Gisse.
Wengine watakao shiriki Redds Miss Ukonga 2012 ni pamoja na
Zawadi Mwambe, Stellah Maurice, Amina Sangawe, Elizabeth Pertty, Alicia
Donatus, Rachel Isaaack na Amina Ramadhani.
Shindano la Miss Ukonga 2012 linadhaminiwa na Redds Primium
Cold, Clouds FM, Father Kidevu Blog, Kiota Jungle, V Mask Logistic, Mambya
Insurance, Mamushka Pub & Catering, Hill tech Resort, Mr Mabaga, G Obonyo
na Excel Beaut Salon.
No comments:
Post a Comment