kabesejr blog

kabesejr

albino

Tuesday, May 15

TATHMINI YA MDAU Revo alex JUU YA MCHEZO WA AL AHLY SHANDY NA SIMBA.



Hii ni kwa mujibu wa mtazamo wangu jamani nikiwa kama Mtanzania niliyeuangalia mchezo ule kwa umakini sana huku nikiwa na matumaini makubwa na Wawakilishi wetu wa pekee waliokuwa wamesalia kwenye mashindano ya kimatafaifa.
(Score zote ni out of 10)
  1. Juma Kaseja

Bila shaka wakiambiwa huyu ndo Tanzania One watasema bado kama nchi hatujajaliwa mtu mwenye kipaji kizuri katika nafasi hiyo kwa kipindi hiki tulicho nacho licha ya kuokoa michomo kama 2,3 iliyoonekana kuwa na madhara makubwa kwa team yake ndani ya dk 90 hakuwa na la ziada, na hata beki yake ilivyopoteza dira kipindi cha 2 hakuonyesha jitihada zozote binafsi za kuzuia madhara kwa team yake,mipira iliyogonga besela na ile iliyokuwa inatoka nje baada ya kumpita inadhihirisha hili,hata ujasiri wake wa kudaka michomo ya penalt tunaoufahamu jana haukuonekana,upande wa kulia alikuwa haendi kabisa na Jamaa walivyogundua hilo wakawa wanampelekea hukohuko, na ndo aliyepiga penalt ya 9 ambayo ilidakwa na kipa wa Shandy na kuitoa team mashindanoni.

Anapata 5
2.Shomari Kapombe

Dogo huyu aliyeko kwenye form alicheza vizuri hasa katika kipindi cha kwanza, baada ya Ahly Shandy kuja na Plan B kipindi cha 2 alizidiwa ukichukulia namba 7 anzia Uhuru na hata alipoingia Machaku walikuwa hawashuki kumsaidia kiasi kwamba mipira mingi iliyoonekana kuwa na madhara makubwa kwa Simba ilikuwa ikipitia upande wake kitendo kinachoweza kuwa kimetia doa deal yake ya kwenda TP Mazembe kama tetesi zilivyokuwa zimezagaa.
Anapata 6
3.Amir Maftah

Alicheza kama beki 3,aliendelea kuwa ni yuleyule tuliyemzoea hakuwa na jipya sana na hakuonyesha kupanda kusaidia mashambulizi kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye baadhi ya mechi za hapa nyumbani labda alicheza kwa kufata maelekezo ya kocha wake wakihofiwa kufungwa.
Anapata 5
4.Victor Costa

Alionekana kucheza kwa kujiamini sana kipindi cha kwanza wakati Simba walivyofanikiwa kuwabana Shandy na kupunguza mashambulizi yao,kibao kilivyogeuka kama ilivyokuwa kwa beki line nzima alichemsha,na ni yeye aliyezembea ku’clear pass iliyomfikia mfungaji wa goal la 3.
Anapata 4
5.Kelvin Yondani

Alikuwa ni yuleyule tunayemfahamu,alicheza vizuri lkn na makosa mawili matatu kama ilivyo kawaida yake.
Anapata 5
6.Mwinyi Kazimoto

Alianza kucheza kama namba 6,baada ya Simba kufungwa magoli ya fasterX2 kocha alimbadilisha namba na Mafisango,pamoja na kujitahidi kufurukuta haikusaidia.
Anapata 5
7.Uhuru Seleman:

Moja ya shambulizi makini la Simba liliishia mguuni mwake,shuti alilopiga kama si umahiri wa kipa wa Ahly Shandy lingeweza kuwapa Simba goli,hata hivyo pass nyingi alizokuwa akipiga zilikuwa zikinaswa na wachezaji wa Ahly Shandy na haikuwa ajabu kocha kumtoa.

Anapata 4

8.Patrick Mafisango:

Alianza kucheza kama kiungo mshambuliaji(labda wakiamini atawabeba kama ambavyo amekuwa akiwabeba kwenye baadhi ya michezo ya ligi iliyomalizika hivi karibuni) baada ya Simba kufungwa goli za 2 za fasterX2 walibadilishana na Kazimoto hata hivyo haikusaidia,still bado Jamaa walikuwa wanawapumulia kila wakati.
Kama ilivyokuwa katika mechi ya Dar, penalt yake iliyookolewa na kipa wa Shandy ndo iliyoendelea kuwaweka Waarabu wale mchezoni.

Anapata 4
9.Felix Mumba Sunzu

Alicheza nyuma ya Okwi,alijitahidi kufurukuta,alikuwa anaonekana ni hatari kuliko washambuliaji wengine waliopangwa katika mechi ile lkn kama inavyokuwaga kwa Mwape wa Yanga hakuwa na jipya.
Anapata 6
10.Emanuel Okwi:

Haikuwa rahisi kuamini kwamba Okwi yule aliyekuwa gumzo katika magazeti yote ya Sudan alikuwepo katika ile mechi,wa’Sudan walianza kwa kumkaba sana labda wakikumbuka jinsi alivyowaadhiri hapa Dsm lakini baada ya muda fulani waligundua alikuwa ni “kapi” wakaachana naye na kuhamishia concentration zao kwa Sunzu aliyeonekana kidogo ni hatari,hakuonyesha kuwa yeye ni professional footballer kwa kubishana na refa bila sababu za msingi kiasi kwamba refa angekuwa ni Israel Nkongo wa Azam angemlima kadi 2 za njano kisha nyekundu,hata hivyo aliambulia 1 ya njano ambayo ilikuwa ni ya kujitakia.
Kwaufupi alikuwa ni Okwi yule wa kipindi cha katikati nyuma( wa leo kucheza vizuri, kesho kuboronga) hakuwa Okwi huyu wa kipindi hiki cha hivi karibuni.
Anapata 3.
11.Haruna Moshi (wenyewe humuita Boban)

Jinsi alivyoingia safarini na Malapa niliamini akili yake haiku sawa na hivyo asingekuwa na lolote la ziada kwa manufaa ya team yake kiwanjani,na ndicho kilichotokea.
Anapata 4


Generally team kama team jana ilifia kwa Okwi,kama wewe ni mfatiliaji wa soka la bongo utakubaliana na mimi kuwa mafanikio ya Simba kwa siku za hivi karibuni kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitengenezwa na jitihada binafsi za Okwi,kwahiyo kitendo cha Okwi kuwa "out of form" jana ndo kiliifanya Simba ya jana ionekane tofauti na ile Simba ya kwenye mechi ya kwanza Dsm.
Ushauri wangu:
Wakati wa kucheza soka kwa kutegemea mchezaji mmoja/wawili umekwisha,Simba inatakiwa kusajili kama kweli wanataka kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa (hii ya nyumbani longolongo za hapa na pale zinaweza kuendelea kuibeba),tofauti na hapo hata Yanga inaweza kujikuta inajipozea machungu hapo kwenye Kagame.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...