Stori na Sifael PaulNI juu ya kilichompata alipotekwa na
watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka amefunguka kuwa alinusa
kifo.
Akisimulia tukio hilo, Dk. Ulimboka alisema kuwa alipigiwa simu na mtu
aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea
naye, ndipo walipopanga kuonana kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni,
Dar.
Dk. Ulimboka aliyekuwa akizungumza kwa tabu, alisimulia kuwa wakati
akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa wakifahamiana naye kabla, alikuwa na
wasiwasi kwani kila mara mtu huyo alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu
wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Dk. Ulimboka alisema kuwa baada ya muda
alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha
wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha polisi na kumvuta na kumuangusha
barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka
naye.
Dk. Ulimboka alisema kuwa, wakiwa njiani walimpiga na kumfikisha katika
Msitu wa Pande na kuendelea kumpiga mpaka alipopoteza fahamu.
Ilielezwa kuwa
jamaa hao walimwacha na kuondoka wakiwa na uhakika kuwa amekufa kumbe alikuwa
amepoteza fahamu tu hadi alipookotwa asubuhi.Chanzo:www.globapublishers.info
No comments:
Post a Comment