Na Shakoor Jongo
Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo, Risasi Jumamosi linafunguka.
ALIJISIKIAJE?
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi Alhamisi ndani ya Ofisi za Global Publishers, Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu’ kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.
TUJIUNGE NA WEMA AKITIRIRIKA!
“Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so’ sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
“Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom’ alipitiliza.”
ALITAKIWA KUHARIRIWA?
“Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya.”
KANITIA AIBU!
“Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo’ kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.
“Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.
“Baada ya kuona nipo kimya ‘aithinki’ siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu.”
TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
“Yaah…ukweli ‘situwesheni’ haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize.”
VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
“Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz’ sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye.”
NISAMEHENI SANA
“Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana. Yaani magazeti ya Global naombeni muwe wa kwanza kunisamehe kwani yule ni mzazi wangu pamoja na yote, nampenda sana.”
NENO LA RISASI JUMAMOSI
Wema ameamua kutoa la moyoni mwake akiamini kuwa yeye ni staa kwa hiyo ni kioo cha jamii, hataki kuwepo na chuki kati yake na vyombo vya habari, kwa maana hiyo AMESAMEHEWA.
Chanzo:www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment