Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dkt. Fenella Mukangara (pichani)
amepata ajali mbaya mchana huu maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati akiwa njiani
kuelekea Jijini Mwanza kwenye Ufungunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo
Vishale (Darts) yanazinduliwa leo Jijini humo.
Globu
ya Jamii imefanya mawasiliano na Mh. Mukangara na kuthibitisha kupata ajali hiyo
ambapo anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo
hakulitaja jina lake).
"Ni
kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani
kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya
Mchezo wa Darts,tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka
katika sehemu mbali mbali za mwili."Alisema Mh. Mukangara.
source:jamii.com
No comments:
Post a Comment