LVIV, Ukraine
BEO pekee la Mario Gomez lilitosha
kuipa Ujerumani ushindi wa 1-0 usiku huu dhidi ya Ureno katika mechi ya Kundi B
ya Kombe la mataifa ya Ulaya mjini hapa.
Gomez alifunga bao hilo, muda
mfupi baada ya kumpisha uwanjani Miroslav Klose,
ambaye alikuwa tayari kwenye mstari wa kuingia uwanjani, wakati anaiwahi krosi
ya Sami
Khedira dakika ya 72 na kuitupia nyavuni.
Gomez |
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alichelewa kufanya
mabadiliko hayo baada ya bao hilo na Gomez alikaribia kufunga bao lingine kabla
ya kutolewa dakika ya 80 akicheza siku ambayo anasherehekea miaka 34 ya kuzaliwa
kwake.
Nani aligongesha mwamba dakika
ya 84th, ikiwa ni mara ya pili Ureno kufanya hivyo kwenye lango la wapinzani wao
hao. Shuti la Silvestre Varela lilikwenda moja kwa moja kwa kipa wa
Ujerumani, Manuel
Neuer dakika ya 89.
Ujerumani walitawala mchezo na
kutengeneza nafasi kadhaa, Pepe alipata nafasi nzuri kipindi cha kwanza, na
mpira mwamba wa chini wa lango la Ujerumani wakati akiujaribu kuunganisha kona
kabla ya mpira kutoka nje.
Licha ya kusema kabla ya mechi
hiyo kwamba atawaanzisha mkongwe Klose kama mshambuliaji, Loew alimtanguliza
Gomez.
Katika hatua nyingine ambayo
haikutarajiwa, Loew pia alimchezesha Mats
Hummels katika beki ya kati badala ya Per Mertesacker.
Mertesacker na Klose wameingia
kwenye michuano hiyo baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu. Mertesacker alicheza
mechi mbili tu za kirafiki baada ya kufanyiwa upasuaji Februari, mwaka huu na
Klose pia alicheza kidogo baada ya kuumia Machi. Mshambuliaji huyo pia
alilalamikia maumivu ya mgongo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Jerome Boateng alicheza
beki ya kulia na pia Loew amesikitishwa na habari za magazeti kuhusu maisha yake
ya usiku.
IMwishoni, ilidhihirika uamuzi
wa Loew ulikuwa sahihi. Hummels alicheza vizuri, Boateng alifanya kazi nzuri ya
kumdhibiti Cristiano Ronaldo na Gomez alifunga bao muhimu.
No comments:
Post a Comment