Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah. |
Na Prince
Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watafungua dimba na Atletico ya
Burundi katika mchezo wa Kundi C wa michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A,
wataanza na URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi wengine wa
Tanzania katika michuano hiyo, Azam FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar
katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Chamazi, Julai 15.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema katika
Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Ilala, Dar es Salaam kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) itashiriki kama timu mualikwa.
Aidha, habari za kusikitisha
ni kwamba, Musonye amesema Sudan, Ethiopia, Eritrea na Somalia hazitaleta
wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
Wakati Ethiopia ligi yao
inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi wao wapo kwenye michuano ya Afrika na
wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia wawakilishi wao Elman wamebadilisha
uongozi, hivyo bado hawajajipanga na Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji
wao kuzamia kila wanapokuja kwenye mashindano, wameondolewa.
“Wameondolewa, kwa sababu
mbili, kwanza nchi yao imeomba ipewe muda kulifanyia kazi sual hilo, na sisi pia
(CECAFA) tunalitafutia ufumbuzi,”alisema Musonye.
Lakini Musonye amekiri kitendo
cha kuyatoa mashindano hayo mwanzoni mwa mwaka hadi katikati ya mwaka
kumechangia baadhi ya timu kutoshiriki na amesema tayari amewasilisha pendekezo
kwenye Mkutano Mkuu, mashindano yarejee kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama
ilivyokuwa awali.
Kuhusu mechi ya ufunguzi ya
Simba kuchezwa Julai 16, ambayo itakuwa Jumatatu badala ya Jumapili, Musonye
alisema kwamba imetokana na kwamba Julai 15, Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali
za Copa Coca Cola, ambayo maandalizi yake yote yamekamilika.
Yanga ndiye bingwa mtetezi wa
mashindano, baada ya kuifunga Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
RATIBA
KAMILI KOMBE LA KAGAME
No comments:
Post a Comment