Msanii mkongwe nchini Dudu Baya anadaiwa kumpiga
mtangazaji wa kituo cha radio cha Kiss FM Ezden chenye makao yake jijini Mwanza,
Ezden Jumanne aka The Rocker.
Akiongea kwa simu na Bongo 5, Ezden amesema issue
ilianza kabla ya ijumaa iliyopita ambapo alikuwa ameandaa show iitwayo Mwanza
Blast iliyoendana na uzinduzi wa mixtape ya rapper Nash MC iitwayo ‘Mzimu wa
Shaaban Robert’.
Amesema baada ya Dudubaya ambaye kwa sasa yupo Mwanza
kuona matangazo ya show hiyo alianza kuponda mtaani kuwa show hiyo haina maana
na ‘itakula za uso.’
Ezden amesema kitendo cha yeye kutomjumuisha kwenye
roaster ya waliopanda kwenye show hiyo kilimuuma.
Dudu Baya aliamua kumtafuta Dj John wa Radio Free
Africa kumuomba nafasi ya kupanda kwenye stage ya show hiyo kwa malipo kiduchu
lakini alikataa na kumwambia amtafute Ezden kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa kila
kitu
No comments:
Post a Comment