ANGALIA JINSI DIAMOND ALIVYOKUWA AMEJIANDAA KWA SHOO YA "DIAMOND ARE FOREVER" NA MASHABIKI ZAKE
UKIZUNGUMZIA
shoo kali zilizoteka mioyo ya mashabiki hapa nchini na ukaacha
kuizubgumzia shoo iliyopigwa usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam,
basi utakuwa hufuatilii kwa makini burudani zinazofanyika Bongo.
Shoo
ya “Diamond Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga
kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati nyingi zilizowahi kufanyika
hapa jijini Dar.
Shoo
hiyo ilipigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita
‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya
mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka
2006 na mcheza filimu,Wema Isaac Sepetu.
Diamond
alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya
elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.
Pamoja
na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa
Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine
kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.
Diamond akiwa jukwaani
Mwanamitindo , Martin Kadinda katika pozi, na huyu
ndiye aliyemvalisha
No comments:
Post a Comment