Diamond anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza uongo mwingi dhidi yake.
Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea…. ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.
Diamond amesema “kuna vitu vya chinichini alikua ananifanyia vya kuniumiza kama kudanganyana lakini nilikua sivipeleki kwenye vyombo vya habari kwa sababu nilikua namuheshimu namfichia kwa sababu anasema hafanyi hivyo, lakini akawa anaendelea kuvifanya kama kunidanganya kwenye mapenzi japo kudanganyana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida hata wapenzi wangu wa zamani walikua wananidanganya na mimi nawadanganya pia, lakini alikua anapeleka kila kitu kwenye magazeti hata vitu vya watu wawili ndani ya nyumba anavipeleka, sasa nyumba inakua haina siri”
“Wema alikua anapeleka stori kabisa yani kitu tumefanya watu wawili ndani unashangaa kukikuta kwenye gazeti, nikikutana na waandishi ambao ni rafiki zangu wananiambia ebwana wewe unajisumbua bure yeye mwenzako akija hapa ndio anataka aandikwe, mimi nilishawahi kumkuta hotelini uchi kabisa akiwa na mwanaume mwingine hotelini mwishoni mwa mwaka jana lakini sikuongea chochote kwenye vyombo vya habari, nikamchukua na kuondoka, niliamua kumtunzia siri yake na nikanyamaza kwa kuichukulia kama mwanaume, na hata nikawa nikifika kwenye media nilikua nampamba na kumtetea kwamba jamani Wema hayuko hivyo na ni mstaarabu”
Diamond amefunga mjadala wa yeye na Wema kwa kuthibitisha kwamba hana ugomvi na Wema wala hana tena hisia za kimapenzi kwa mshindi huyo wa Miss Tanzania 2006, hawezi kurudiana nae kwa sababu kwa sasa imetosha na anampenzi mwingine ambae hata Wema anamfahamu.
Ishu yote hii imetokana na show aliyoifanya Diamond pale Mlimani City weekend iliyopita ambapo Diamond alikataa kupokea pesa Wema Sepetu aliyokua anampa pale kwenye stage kwa sababu ya kukwepa Drama, Na Wema hakua mpenzi pekee wa zamani wa Diamond aliekuwepo kwenye show, kulikua na warembo wengine wawili wa zamani wa Diamond lakini hao wote alipokea pesa zao.
Uhusiano wa Diamond na Wema umedumu kwa mwaka mmoja ambapo walipanga kuoana huku tayari Diamond akiwa amemvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambae pia ni mwigizaji wa movie Tanzania.
Diamond amethibitisha kwamba Show yake ya DIAMONDS ARE FOREVER siku tatu kabla ya kufanyika, tayari ilikua imeuza ticket zote elfu moja na hivyo ukumbi kujaa, huku kila ticket ikiwa ni shilingi elfu 50…… show yake imekua show ya kwanza ya msanii wa kibongo kulipisha watu elfu 50 na bado ikajaza mpaka watu wakakosa ticket, kwa swala la kiingilio amezishinda mpaka show za Jay Z & 50 cent ambazo zilifanyika bongo na watu kulipa elfu 25 – 30.
No comments:
Post a Comment