Joyce Banda
Makamu wa rais wa Malawi Joyce Banda ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kifo cha rais Bingu wa Mutharika ambapo Banda anakuwa rais wa kwanza wa kike kusini mwa Jangwa la Sahara, na aliapishwa mbele ya bunge katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.
Joyce ambae amekuwa makamu wa rais tangu mwaka 2009, alishangiliwa na kupigiwa makofi kabla na baada ya kutangazwa.
Kuchelewa kutangazwa kwa kifo cha Mutharika kulisababisha wasiwasi kuhusu nani anaongoza nchi hiyo, na Kulikuwa na tetesi kuwa watu wa karibu wa rais Mutharika walikuwa wakitaka kubadili katiba ya nchi ili kuzuia Joyce Banda kuchukua madaraka, na badala yake kumpa ndugu yake, Peter Mutharika ambaye ni waziri wa mambo ya nje.
BBC wamesema kwamba Joyce Banda alifarakana na rais Mutharika mwaka 2010 na kuwa mkosoaji mkubwa wa rais ambapo Alifukuzwa kutoka chama cha DPP na kuunda chama chake cha Peoples Party |
No comments:
Post a Comment