Aprili 24,
2012
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi wane wa Tanzania kuchezesha mechi ya marudiano ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Black Leopards ya Afrika Kusini na Warri Wolves ya Nigeria itakayochezwa nchini Afrika Kusini kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Waamuzi hao
ni Waziri Sheha atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa John
Kanyenye na Erasmo Jesse. Mwamuzi wa akiba (fourth official) atakuwa Israel
Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Aurelio Mathias wa Msumbiji.
Mechi ya
kwanza kati ya timu hizo itachezwa Jumapili (Aprili 29 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Warri City ulioko Jimbo la Delta nchini Nigeria na itachezeshwa na waamuzi
kutoka Senegal wakati Kamishna atakuwa Inyangi Bokinda wa Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo (DRC).
1,635
WASHUHUDIA MECHI YA YANGA, POLISI DODOMA
Mechi ya Ligi
Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Polisi Dodoma iliyochezwa (Aprili 22 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilishuhudiwa na watazamaji 1,635 na
kuingiza sh. 5,666,000.
Baada ya
kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) ambayo ni sh. 864,305.08 kila klabu ilipata sh. 193,858.47, uwanja sh.
26,469.49.
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 26,469.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 108,687.80. Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
sh. 13,234.75, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 2,646.95 na asilimia 10 ya
gharama za mechi ni sh. 26,469.49.
Gharama za
awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani
kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya
kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 1,500,000,
usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 1,500,000 na Wachina (Beijing Construction) sh.
1,000,000.
Kutokana na
mechi hiyo kuingiza kiasi kidogo baadhi ya gharama zililipwa nusu au kutolipwa
kabisa na kuacha madeni. Madeni hayo ni tiketi sh. 1,500,000, maandalizi ya
uwanja (pitch marking) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa
uwanja sh. 850,000 na Wachina sh. 1,000,000.
POLISI MORO,
MGAMBO, PRISONS ZAPANDA VPL
Fainali ya
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyoshirikisha timu tisa imemalizika jana (Aprili
23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku tatu zikifuzu kucheza
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2012/2013 utakaonza Agosti mwaka
huu.
Timu hizo ni
Polisi Morogoro iliyofikisha pointi 20 ikifuatiwa na Mgambo Shooting ya Tanga
(15) na Tanzania Prisons ya Mbeya iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na
pointi 14.
Nyingine
zilizofuatia na pointi zao kwenye mabano ni Polisi Dar es Salaam (13), Mbeya
City Council (11), Rhino Rangers ya Tabora (8), Mlale JKT ya Ruvuma (8), Polisi
Tabora (6) na Transit Camp ya Dar es Salaam (2).
SIMBA, MORO
UNITED ZAINGIZA MIL 28/-
Pambano la
Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Moro United lililochezwa jana (Aprili 23
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
28,688,000.
Jumla ya
watazamaji 7,945 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh.
3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 6,946 kati ya hao
walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya
kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) ambayo ni sh. 4,376,135.59 kila klabu ilipata sh. 4,919,009.32, uwanja sh.
1,454,286.44.
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,058,414.58, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 727,143.22, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 145,428.64 na
asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 1,454,286.44.
Gharama za
awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani
kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya
kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 80,000, gharama ya tiketi sh. 3,000,000,
maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa
uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Nayo mechi kati ya Villa Squad na African Lyon iliyochezwa Aprili 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam iliingiza sh. 496,000 ambapo kila klabu ilipata sh. 68,061.70 wakati watazamaji walioshuhudia mechi hiyo ni 469.
Vilevile mechi kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan iliyochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 9,717,000 kutokana na washabiki 2,562.
MECHI ZA LIGI
KUU WIKIENDI HII
Ligi Kuu ya
Vodacom imeingia raundi ya 25 ambapo kesho (Aprili 25 mwaka huu) Oljoro JKT
itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa
Chamazi, Dar es Salaam.
Raundi hiyo
itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28 mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa
mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam na Toto
African zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka huu Villa
Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo
itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa
uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh
Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini,
Mlandizi).
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga),
African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar
es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment