Habari: Mashaka Baltazr wa Global Publisher, Mwanza
SALMA
Hamidu, mkazi wa Igogo, jijini Mwanza ameibuka na kudai amezaa na
marehemu Steven Kanumba mtoto wa kike aitwaye Treasure Steven Charles
Kanumba (2), Ijumaa linashuka na maneno ya kinywa chake.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Salma anayefanya kazi kwenye Ofisi ya Uwakili ya Law
Consultancy jijini Mwanza, alidai alianza kufahamiana na marehemu mwaka
2006 wakati yeye akiwa kwenye Kundi la Nyakato Arts chini ya Mwalimu
Joseph.
CHANZO CHA UHUSIANO
Salma
akasema kuwa, uhusiano wao uliunganishwa na Mwalimu Joseph ambaye
alimpa marehemu namba zake za simu wakati alipopeleka filamu za Machozi
Yangu na Siri Yangu kuifanyia uhariri (editing) jijini Dar es Salaam
katika studio alizokuwa akifanyia kazi marehemu.
“Marehemu
alipoona picha zangu kwenye filamu hizo alivutiwa na mimi katika
kuigiza, akaomba namba zangu za simu kwa Mwalimu Joseph,” alisema Salma.
Mrembo
huyo aliendelea kuweka wazi kuwa, baadaye Mwalimu Joseph alirejea
Mwanza na kumtaka radhi kwa kumwambia alimpa Kanumba namba zake za simu.
SIMU YA KWANZA YA KANUMBA KWA SALMA
“Baada ya wiki mbili nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Kanumba. Aliuliza kama huwa nasafirisafiri.
“Nilimjibu
si sana kwa sababu nasoma. Wakati huo nilikuwa nasomea kompyuta kwenye
Chuo cha English Kingdom Nyakato,” alisema Salma.
Akaongeza:
Marehemu alinielewa, lakini akaniomba niwe mwenyeji wake punde
atakapokuja Mwanza, nikaridhia ombi lake, alikata simu, lakini
tukaendelea kuwasiliana kwa simu kila mara.
Salma alisema mawasiliano yake na Kanumba yalidumu kwa mwaka mmoja bila kuonana ‘laivu’.
Aidha,
alidai kuwa siku moja marehemu alimpigia simu akimtaka kujiunga na
kundi lake lililopo Dar, akamkubalia lakini tatizo likawa umbali.
“Lakini marehemu akaniambia nisiwe na wasiwasi kuhusu hilo,” alisema
Salma.
Akizidi kumwaga data za uhusiano wao ulivyoanza, Salma alisema:
(Salma Hamidu aliyezaa na marehemu Steve Kanumba.)
LAIVU KWA MARA YA KWANZA
“Mwaka
2007, Kanumba aliniita Dar, alinitumia tiketi ya ndege ya Precision
Air, kwetu niliaga nakwenda kumsalimia mama mkubwa anayeishi Tabata.
“Nilipofika
Dar, nilimpigia simu Kanumba kumtaarifu nimefika, akanitaka tukutane
Ubungo Plaza Hotel (Blue Pearl),” alisema Salma.
Pale
Ubungo Plaza, marehemu kwa mara ya kwanza alimtamkia lililo moyoni
mwake kwamba ametokea kumpenda na akamuomba wawe wapenzi.
“Sikuwa na uamuzi wa haraka, lakini kutokana na ushawishi wake nilikubali, baadaye nilirudi Tabata kwa mama mkubwa.
“Usiku
alinipigia simu, akaniomba kesho yake tusafiri kwenda Zanzibar,
nilikubali, asubuhi niliaga kwa shangaza tukaenda Zanzibar.
“Tulifikia
Bwawani Hoteli. Tulikaa kwa siku tatu na kwa mara ya kwanza nilikutana
na marehemu kimwili. Tuliporudi Dar mimi nikarejea Mwanza,” alisema
Salma.
KANUMBA PENZI LAKOLEA, ATUA MWANZA
“Baada
ya kama miezi minne na siku kadhaa hivi, marehemu alinipigia simu
akasema yuko Mwanza, anataka kuja chuoni kuniona. Alikuja akiwa
ameongozana na marafiki zake wawili, Credo na Theonist Rutashoborwa.
“Walikuja
hadi chuoni, mimi nilitoka tukaenda kukaa kwenye baa ya Shentemba.
Ilipofika saa 2 usiku, tukahamia Isamo Hotel,” alisema Salma.
Salma
aliendelea kusema kuwa, pale Isamo walipata chakula kabla ya kujitupa
kitandani lakini siku hiyo muda mwingi alikuwa akijisikia vibaya,
marehemu akamtaka asubuhi akapime.
“Asubuhi
nilikwenda kwenye Kliniki ya Dokta Ng’walida, daktari bingwa wa
magonjwa ya akina mama na watoto. Vipimo vilionesha nilikuwa na ujauzito
wa miezi minne.
“Nilimwonesha
marehemu majibu yale, hakuonekana kukubali wala kukataa, lakini baadaye
akasema kazi yake haimruhusu kuwa na mtoto wala familia hadi
atakaponiambia.
“Baada
ya siku mbili, aliaga kurejea Dar pamoja na marafiki zake. Siku chache
baadaye huku nyuma kwa bahati mbaya ujauzito ulitoka, nilikwenda kwa
daktari mmoja Nyakato National ambaye alithibitisha hilo. Huo ulikuwa
mwaka 2008.
UJAUZITO WA PILI
Salma alisema kuwa mawasiliano na marehemu yaliendelea. Kuna siku alimpigia simu akimtaka wakutane jijini Arusha.
Alipofika alipokelewa na Kanumba mwenyewe kabla ya kwenda kupiga kambi kwa rafiki yake mmoja aliyekuwa akiishi peke yake.
Akasema kukutana kwao kimwili kwa safari hii, ndiko kulimpa ujauzito na hatimaye kujifungua binti anayeitwa Treasure au Tunu.
Arusha
waliondoka na ndege hadi Mwanza ambapo walifikia Ladson Hotel, ipo
Bwiru na kukaa kwa siku mbili kabla ya kumruhusu kurejea nyumbani kwao
Igoma.
Akiwa na ujauzito huo, Kanumba alimtumia nauli akimtaka wakutane mjini Morogoro.
“Nikiwa
na tumbo langu, aliniita Morogoro, nilisafiri kwa basi hadi kule,
nilifikia kwa shangazi yangu yeye alipanga kwenye hoteli ipo jirani na
Kituo cha Mabasi cha Msamvu.
KANUMBA ATOA ONYO
“Kulitokea
kutokuelewana kidogo na marehemu kwa sababu ya ujauzito ule, akirejea
mazungumzo yake ya awali kuwa, kazi yake haimruhusu kuwa na mtoto wala
familia, lakini nilimwambia sina namna ya kufanya kuhusu ujauzito ule.
“Hata
hivyo, marehemu alinionya nisimwambie mtu kuhusu ujauzito kuwa ni wa
kwake, iwe siri yangu na yake kwa sababu hakutaka habari hiyo ifike
kwenye magazeti,”alisema Salma.
Akaongeza: Baada ya hapo, alinipa shilingi 150,000 nikarudi nyumbani Mwanza.
“Nikiwa
Mwanza alikuwa akinipigia simu akitaka kujua naendeleaje na tumbo langu
na kunitaka nijiandae kwa safari ya Dar, atanitumia tiketi ya ndege.
“Nilisafiri,
nilipofika Dar nilimjulisha, akasema tusikae Dar, twende Zanzibar. Kule
tulifikia tena Bwawani Hotel. Tulikaa kwa siku nne, kisha tukarejea
Dar.
Lakini
tukiwa Zanzibar kuna mtu alinipigia simu na yeye akiwepo, alikasirika
sana na kuninyang’anya simu, akachukua namba kisha akampigia mtu huyo,
waligombana kwenye simu. Aliipasua simu yangu, akaenda kuninunulia
nyingine.
“Alikuwa
mtu mwenye hasira, hakutaka kusikia unazungumza na simu hasa ikiwa ni
sauti ya kiume. Ugomvi huo ulisababisha aikane mimba, akasema
namsingizia ni ya mwanaume aliyenipigia simu. Ilifika mahali akasema
kila mtu aishi kivyake.
“Hata hivyo, alikuja kuniomba msamaha huku akizidi kunionya kuwa ole wangu nitangaze nina mimba yake.”
Alisema
ugomvi wake na Kanumba ulitokana na ujauzito na ilifika mahali Salma
alimweleza mama yake ambaye alimlaumu kwa kujiingiza kwenye uhusiano na
mwanaume huyo.
MISAADA KUTOKA KWA KANUMBA
Kwa
upande wa misaada, Salma alisema akiwa mjamzito, marehemu alimtumia
shilingi Milioni mbili na laki mbili kwa ajili ya kununua kiwanja.
Baadaye
alimtumia shilingi Milioni moja za kupanga nyumba. Fedha hizo alizituma
kupitia Benki ya Standard Chartered Tawi la Mwanza.
Baada
ya kutuma fedha hizo, marehemu aliwahi kwenda Mwanza na kufikia kwenye
Hoteli ya Ryans Bay. Wakati huo mimba ilikuwa na umri wa miezi saba.
HAKUTAKA KUPIGA NAYE PICHA
Salma
anasema: Nilimtaka tupige picha ya ukumbusho akakataa, lakini
nilipojifungua alikuja na kumpiga picha mtoto kwa kutumia simu yake
akisema, ‘mtoto mama yangu mtupu kwani amefanana naye sana.’
Aliongeza
kuwa alipojifungua Kanumba alimtumia shilingi 500,000 za matumizi ya
mtoto kupitia simu ya mama yake mzazi na Salma (hakumtaja jina).
Aliendelea
kusema kulijitokeza sakata wakati wa kumpa jina mtoto, Kanumba akitaka
amwite jina la mama yake, huku Salma naye akitaka kumwita la mama yake,
ndipo wakakubaliana mtoto aitwe Treasure au Tunu ili kumaliza mzozo wa
kugombea kumwita mtoto jina la upande mmoja.
“Treasure
alipofikisha miezi saba alisema nimpige picha nimtumie ili amwone
alivyofikia, nilifanya hivyo. Siku moja akaniambia angetunga filamu
kuhusu maisha yetu ambayo alipendekeza iitwe My Gift.“Siku
chache kabla ya kifo chake alinipigia simu pamoja na mtoto akisema
alitaka kusafiri na asingekuwepo kwa mwezi wote wa Machi mwaka huu,
alimsamilia mwanaye. Lakini cha kushangaza siku chache nikapewa taarifa
za kifo chake,” alisema Salma.
KWA NINI USIRI?
Salma
alisema mpaka sasa anashindwa kuelewa ni kwa nini marehemu alitaka
uhusiano wao uwe wa siri. Lakini baadhi ya marafiki zake walikuwa
wakifahamu uhusiano huo.
NENO LA MWISHO LA SALMA
“Kanumba
kaniacha njia panda, sijui la kufanya, lakini ni vyema kama
angemtambulisha mwanaye kwa ndugu zake kuliko hivi sasa ambapo mengi
yatazuka kuwa pengine natafuta fedha za marehemu.“Sijaweka wazi ili nipate chochote, bali nahisi dhambi kuficha kwa sababu huyu mtoto si damu yangu peke yangu.“Nitakuwa
mbaya kwa Mungu kama nisiposema ukweli. Angekuwepo mwenyewe nisingesema
kwa sababu yeye ndiye alikuwa kiongozi wa maisha ya mtoto.“Narudia
tena, nina uwezo wa kumlea na wala sihitaji mtoto achukuliwe na kwenda
kuishi kwa baba, ila familia ijue kuna damu yao kwangu.“Kama hawataamini, niko tayari kufika Dar na kupima DNA ili familia ya marehemu ijiridhishe,” alisema Salma.Hata
hivyo, Salma alikiri kufanya kosa la kutowahusisha marafiki wa Kanumba
kumtegulia kitendawili hicho na kudai pengine umri mdogo ulichangia.
Salma alizaliwa mwaka 1987.Alisema
mtu pekee ambaye watu wanamfahamu na ndiye shahidi wa uhusiano wake na
marehemu ni msanii wa maigizo, Ramadhan Malele ‘Swebe’ ambaye alikuwa
akiwasiliana naye mara kwa mara.Salma
alisema kabla Kanumba hajafikwa na mauti, yeye aliwahi kukutana na
Swebe jijini Mwanza ambapo alimsimulia hali ilivyo na akamshauri
kusikiliza matakwa ya marehemu ya kutotoa siri ya kuwepo kwa mtoto huyo
No comments:
Post a Comment