Habari za redio one ambazo zimethibitishwa na Katulanda Frederiki mwandishi wa Mwananchi aliye Dodoma zinasema mawaziri nane wameamua kuachia ngazi usiku huu.
Mawaziri hao ni; Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.Tutaleta habari hii uthibitisho usionamashaka utakapojulikana asubuhi.
No comments:
Post a Comment