kabesejr blog

kabesejr

albino

Wednesday, April 18

RONALDO AITAJA MADRID NA BARCELONA KUA TIMU NZURI KWAKE

 

Akiwa na miaka 35, kuna vichache sana ambavyo bado havijazungumzia kuhusu mbrazili Ronaldo. Mafanikio aliyoyapata mtupia nyavuni huyu yanaongea kwa sauti kubwa sana, O Fenomena ndio mfungaji bora wa muda wote wa FIFA World Cup, ameshinda medali mbili za kombe la dunia, ameshinda mara tatu tuzo ya FIFA World Player na mara mbili tuzo ya Ballon d'Or.

Ronaldo ambaye kwa sasa amestaafu soka ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya 2014 FIFA  World Cup.

Pamoja na kuwa busy sana kuitumikia nafasi yake katika kamati hiyo, mchezaji huyo wa zamani wa PSV Eindhoven, Barcelona, Inter Milan, na Real Madrid aliongea na mtandao wa FIFA.com kuhusu career yake, presha iliyopo dhidi ya Selecao na nafasi yake kwenye kombe la dunia la mwaka 2014.

FIFA.com: Kama mmoja ya kamati ya maandalizi ya FIFA World Cup, je una mategemeo yapi kwa michuano hiyo?
Ronaldo: Tunajisikia fahari sana kuandaa kombe la dunia hapa Brazil. Tutakuwa na nafasi kubwa ya kukua, ambayo ni muhimu kutokana wingi wa watu waliopo nchini kwetu ambao wamesongwa na ukosefu wa ajira. Kupitia michuano hii kutakuwa na uwezekezaji mkubwa katika miundombinu. viwanja vya ndege, barabara, hospitali na hoteli. Kutakuwa na manufaa ambayo yatainufaisha Brazil na maisha yetu wote, na hilo linawezekana pekee kwa sababu ya Kombe la dunia.

Unadhani Brazili wapo tayari kwa ajili ya michuano hii?
Kuna mabadiliko makubwa katika kikosi cha timu ya taifa, kizazi kipya ambacho kiukweli bado hakichezi soka zuri bado. Na nafikiri itachukua muda kidogo ili kuweza kufikia kucheza soka la kibrazili asilia. Lakini kati ya sasa na 2014 kuna muda mzuri kupata consistency, kuelewana, na kuwa katika hali ya kuweza kushindana na kuwa na kikosi ambacho kitakuwa na uwezo kulinda heshima ya nyumbani na kuchukua kombe.

Neymar, Alexandre Pato na Ganso ndio wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika kizazi hiki kipya cha Brazil. Je una maoni gani juu watatu hawa?
Ni wachezaji watatu ambao wana vipaji sana, wabrazili ambao wanang'ara katika vilabu vyao. Nadhani Neymar ndio aliyebarikiwa zaidi, na akiwa ndio kwanza ana miaka 19, tayari ameshakuwa na uwezo wa ajabu. Anafunga magoli mengi na tayari ameishakamata Brazil, mashabiki wanampenda. Uzoefu wa kimatifa alioupata katika michauno ya dunia ya vilabu haukuwa mzuri sana, lakini nina hakika bado na muda wa kujifunza zaidi. Pato kwa upande wake, tayari ameshadhirisha kipaji chake barani ulaya, wakati Ganso pia ni mzuri sana  anachohitaji na kupata bahati ya kuepeukanana majeraha.

Unafikiri kuna nafasi kwa wachezaji wazoefu kama Ronaldinho na Kaka?
Ni wachezaji muhimu, ofcourse. Kwa majukumu yao nje ya dimba, na itategemea na fomu zao na kama wanacheza vizuri  kipindi kombe la dunia likiwa linakaribia then wana nafasi. Lakini pia bado wana majukumu nje ya dimba, uzoefu wao utakuwa kitu muhimu kwa ajili ya kikosi ambacho kitakuwa na wachezaji wengi wenye umri mdogo.

Je unaiweka Brazili nafasi ngapi kwa ubora wa soka duniani kwa sasa?
Kiukweli kwa sasa hatupo katika Top 3, lakini nafikiri tupo katika top 5 ya timu bora duniani, hata kama hatupo on fire kwa sasa. Kufanya mabadiliko haijawahi kuwa rahisi na hawa wachezaji wadogo wanahitaji kuimarika. Hakuhitaji kupaniki, wanahitaji kupewa muda ili kufanya vizuri.

Unadhani ni mchezaji gani ambaye unaona ndio mrithi sahihi wa Ronaldo?
Leandro Damiao, kutoka Internationa de Porto. Ni mrefu, ana nguvu, na pia ni mfungaji mzuri, anatisha sana hewani na uwezo mkubwa katika miguu yote miwili. Atkauwa mchezaji muhimu sana katika michuano ya 2014.

Ebu tuangalie siku za nyuma kipindi unacheza soka. Ulicheza Brazil, Spain, Uholanzi na Italy, wapi unadhani kuna mashabiki wenye mapenzi makubwa na soka?
Nafikiri mashabiki wa nchi zote ni vichaa wa soka, japokuwa wana staili tofauti za usangaliaji.

Katika timu zote ulizocheza ni timu gani bado ipo moyoni mwako na itaendela kuwa hivyo?
 Naangalia muda wangu niliokuwa pale Real Madrid jinsi kulivyokuwa na upendo. nafikiri ndio ulikuwa muda wangu mzuri zaidi katika maisha yangu ya soka. Pia nilipenda maisha yangu pale Inter Milan, niliipenda timu na mashabiki wa mji wa Milan.Lakini kote nilipocheza nilikuwa na marafiki wengi na kuwa muda mzuri.

Je safari yako ya kwenda na timu katika World Cup 1994 USA, ilikuwa na umuhimu gani tena ukizingatia ulikuwa na miaka 17?
Ilikuwa muhimu sana. Kuwaona wachezaji wa kariba ya Romario na Bebeto kwa ukaribu na kuwajua vizuri. Niliweza kujifunza mengi kutoka kwao, pia kupata maelezo kadhaa, kama jinsi gani wanafanya mazoezi, na mengine mengi. Romario alikuwa akinituma sana, kama kwenda kumchukulia viatu vyake na kumletea kahawa - yaani kama mwanae vile, lakini siku zote alikuwa akiniheshimu .

Tuambie katika miaka ya sasa ni timu gani inakufurahisha inavyocheza?
Napenda sana jinsi Madrid wanavyocheza soka lao, lakini huwezi kuiacha Barcelona, ambao wana timu nzuri sana. Kila mchezaji wa kila eneo wa anajua nini afanye katika muda muafaka. Pia wana uwezo mkubwa kukaa na mpira huku wakipasiana vizuri kwa kwenda mbele kwenye goli la wapizani. Ni kazi nzuri sana ambayo Pep Guardiola ameifanya, Barcelona ni moja ya timu nzuri sana ambayo nimewahi kuishuhudia katika maisha yangu ndani ya sayari hii. Inauma kusema hivi ukizingatia mimi ni Madridista, lakini nafikiri tunaweza kushinda mataji mbele yao msimu huu.

Haya sasa tutajie perfect eleven yako ya kikosi cha Brazil.
Mmmh hi ngumu kidogo lakini hawa watastahili. Taffarel, Cafu, Aldair, Lucio, Roberto Carlos, Junior Zico, Rivelino, Pele na mimi mwenyewe. Hi ni timu ya hatari ingeweza kusambaratisha timu yoyote duniani.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...