kabesejr blog

kabesejr

albino

Saturday, April 14

TBL KUDHAMINI TAIFA STARS

 

BIA ya Kilimanjaro Premeum Lager rasmi ndio mdhamini mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Morefire imeipata hiyo.

Bia hiyo inayozalishwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wiki hii itafanya hafa maalum ya kuutangaza rasmi udhamini huo.

Chanzo cha habari kutoka TBL, kimesema hafla hiyo itafanyikia katika hoteli ya Serena, iliyokuwa Royal Palm Movenpick, Dar es Salaam wiki hii.   

Tangu mwaka 2006, Taifa Stars imekuwa ikidhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambao wameshindwa kuingia mkataba mpya na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa sababu ya kupandishiwa dau.  

Baada ya mkataba wao (SBL) kufikia tamati Desemba, mwaka jana, TFF ikaipandishia dau la udhamini kutoka Sh. Bilioni 1.2 hadi Bilioni 3.6, ambayo ni zaidi ya asilimia 300.
TBL imekubali kuidhamini Stars kwa dau la Sh. Bilioni 3.6 kwa mwaka.
Kilimanjaro pia ni wadhamini wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga na mashindano ya Kombe la Taifa, Kili Taifa cup

 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...