kabesejr blog
kabesejr
albino
Saturday, April 21
HALI YA SAJUKI INAZIDI KUDHOOFU
Wiki mbili sasa kupita tangu chama cha wacheza filamu nchini(BONGO MOVIE) kupatwa na majonzi ya kumpoteza mwenzao aliyekuwa nguli katika tasnia hiyo ya filamu marehemu Steven Kanumba, sasa wamekutwa na tatizo lingine la mmoja wa chama hicho bwana Sadick Juma Kilowoko alimaarufu kama Sajuki hali yake kiafya kuzidi kuwa mbaya. Sajuki alianza kuumwa au kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni(Tezi) mwanzoni mwa mwezi Novemba na kutibiwa katika Hospitali ya TMJ iliopo jijni Dar es salaam. Kwasasa hali ya msanii huyo imezidi kuwa hatarishi na kufanya apungue mwili na afya kuwa dhoofu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment