kabesejr blog

kabesejr

albino

Monday, April 30

MBUNGE WA SUMBAWANGA CCM AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA


Jana ndiyo kunatolew hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.

Moja ya kituko katika kesi hii mara baada ya mbunge huyo kuulizwa kama anaamini na kusema hajui kama alishinda ila mkurugenzi ndiye anayejua ushindi huo, kimsingi ulinzi umeimalishwa kwani yaweza kuwa mbaya endapo Aeshy atatangazwa mshindi, askali wapo wa kutosha, washawasha na mabomu, lakini kesi hii ilikosa umaarufu kwa kuwa waandishi njaa wote walikuwa upande wa Aeshy

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...